Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Thursday, October 2, 2014



Gazeti la South China Morning Post linadai kuwa Balozi wa Tanzania nchini China Luteni Generali mstaafu Abdulrahman Shimbo amewatishia
wafungwa wa Kitanzania walioko magerezani Hong Kong kwa
kupatikana na hatia ya kusafirisha madawa ya kulevya nchi humo.
Balozi Shimbo anadaiwa kuwaonya wafungwa hao kuwa familia zao
nchini Tanzania zitakuwa hatarini kama wafungwa hao wataendelea na
kampeni yao ya kuwaonya Watanzania wengine kutojihusisha na
biashara ya madawa ya kulevya.
Mwezi uliopita Balozi Shimbo alifanya zaira katika gereza la Stanley
nchini Hong Kong. "Ziara ya balozi wetu ilikuwa kama janga kwetu"
alisema Gervas, ambaye ni moja ya wafungwa katika gereza la
Stanely." Gervas aliongeza "Ametukatisha tamaa katika kampeni yetu
dhidi ya madawa ya kulevya, ikiwa ni pamoja na kututahadharisha
kuwa tuwe makini au tutahatarisha maisha ya familia zetu Tanzania.
Pia Balozi Shimbo alienda mabli zaidi na kukosoa kampeni zetu
akisema kuwa hazijaleta mabadiliko makubwa".
Hata hivyo, Edmund Kitokezi, ambaye ni afisa katika Ubalozi wa
Tanzania uliopo jijini Beijing, amekanusha kuwa Balozi Shimbo
amewatishia wafungwa hao na kuongeza kuwa badala yake Balozi
aliwapa moyo wa kufunguka zaidi. "Tunaunga mkono kampeni yao - hii
ndiyo position ya serikali. Siyo kazi ya ubalozi kumwambia kila mtu
aachane na hiyo kampeni" alisema Kotokezi.
Watanzania waliofungwa Hong Kong walianza kampeni yao dhidi ya
biashara ya madawa ya kulevya kwa kuandika barua ambazo
zimekuwa zikichapishwa na Padri Fr John Wotherspoon katika tovuti
yake Padri Wotherspoon anatoa huduma za kiimani katika magereza
huko Hong Kong.

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni