Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Thursday, October 2, 2014



Nina uzoefu kidogo na mambo ya kazi za ajira maofisini, nimefanya hivi
kwa muda mrefu. Wakati flani nilifanya kazi katika ofisi zilizo katikati
ya jiji, kule mitaa ya Posta jijini Dar es Salaam.
Ofisi nyingi za serikali na watu binafsi zinapatikana mitaa ile. Kutokana
na sababu hiyo, kuna idadi kubwa pia ya migahawa, hoteli, mama
ntilie, pub na kadhalika.
Kuna mambo mawili makubwa yenye ushawishi mkubwa wa usaliti. Ofa
za chakula au vinywaji na usafiri. Kwa kawaida, wafanyakazi wa ofisi
moja hupenda kutoka pamoja wakati wa chakula cha mchana,
wenyewe tunapendelea zaidi kusema lunch!
Kila mmoja ana sehemu yake anayokula kulingana na kipato chake,
wapo wanaokwenda Southern Sun kupata chakula cha mchana, na
wapo wanaowafuata mama ntilie wanaojibanza kwenye vichochoro
vingi vilivyopo mjini.
Huko ndiko tunakokutana na akina dada waliovalia vizuri na
kupendeza, wakitokea katika maofisi mbalimbali, huwezi kujua yupi ni
mhudumu wa chai, yupi ni bosi, wote wanang’ara. Na hapa ndipo ofa za
misosi zinapoanza kushawishi ngono.
Kijana mmoja mwenye kipato kikubwa ofisini kwake, atavutiwa na
msichana mrembo mwenye mshahara wa wastani. Ili kumsogeza
karibu, atalipia chakula cha siku hiyo na kumualika kwa kesho yake.
Kulipiwa chakula ni jambo dogo, lakini lenye thamani kubwa sana. Si
rahisi mtu aliyekulipia chakula kwa nia njema, ukaacha kumshukuru na
hata kumwelekeza unapofanya kazi.
“Mimi nipo pale Oj Traders,” msichana anaweza kujita mbulisha jina na
kusema anapofanyia kazi huku mkaka akimweleza kuwa yeye ni
mhasibu katika ofisi flani. Watakapo
kutana mara ya pili, wataachiana namba za simu.
Baada ya hapo, mkaka atafanya mbwembwe za kuhamahama maeneo
ya lunch ili mradi tu mdada wa watu aingie kwenye laini.
Ukimaliza suala la lunch, kuna hii kitu foleni, hasa kwa wakazi wa Dar
es Salaam. Raha ya kufanya kazi katikati ya jiji inaingia shubiri kadiri
jioni inavyozidi kusogea. Kuanzia saa kumi, ni vurugu katika vituo vya daladala na hasa wakati kama huu ambao bodaboda zimezuiliwa
kuingia mjini.
Wenye magari binafsi ndiyo wakati wao wa kujidai, ingawa foleni
inawakumba wote. Lakini ni afadhali ukiwa kwenye foleni ndani ya gari
dogo, mko wawili kuliko foleni, umeshika bomba kwenye daladala.
Siyo rahisi kwa mdada kukataa lifti ya kijana mwenye gari. Na katika
foleni ndefu, ni wazi kwamba hadi mwisho wa safari, watakuwa
wameshabadilishana namba. Kwa msichana, kuwa na uhakika wa
usafiri kila siku ni ukombozi.
Tusidanganyane, hakuna msichana ambaye hatajua kuwa lunch au
usafiri anaopewa unahitaji malipo maalum, ambayo ni penzi. Hali hii
haiko Dar tu, bali nchi nzima na pengine duniani kote.
Mwanamke aliyeajiriwa anakuwa katika mitihani mikubwa zaidi ya
kusaliti ndoa au uhusiano wake, kwa sababu hata kama haitakuwa
kwenye chakula au usafiri, bado watu anaokutana nao katika utendaji
wake, wanaweza kumghasi. Fikiria anakutana na mabosi, marafiki wa
mabosi wake, wafanya biashara, atapona kweli?
Hata hivyo, simaanishi kama tabia hii inawakumba waajiriwa wote,
isipokuwa nadhani ni sehemu kubwa wanahusika!
By Mike Tee

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni