Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Thursday, October 2, 2014


KIMENUKA! Habari ya mjini kwa sasa ni bethidei ya Miss Tanzania
2006, Wema Sepetu kutimiza miaka 26 tangu kuzaliwa, lakini ndani ya
tukio hilo, mengine yameibuka!
Miongoni mwa yaliyoibuka kwenye sherehe hiyo iliyofanyika Jumapili
iliyopita nyumbani kwa Wema, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini
Dar es Salaam ni madai ya mama Wema, Mariam Sepetu kudaiwa
kupewa nafasi ya kutoa ‘neno la hekima’ lakini akaitumia
kumvurumishia mitusi aliyekuwa shosti wa Wema, Kajala Masanja.
KUNASWA KWA SAUTI NA PICHA
Baada ya sherehe hiyo, Jumatatu na Jumanne, mitandao mingi ya
kijamii ilitumbukiza video yenye sauti ikimuonesha mama Wema
akimrushia matusi Kajala kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na
kukorofishana kwa mwanaye na Kajala aliyewahi kumfadhili
mahakamani kwa kumlipia faini ya shilingi milioni 13 asiende jela kwa
kesi ya kuuza nyumba iliyokuwa na zuio la kisheria.
KAJALA AAMUA ZITO
Katika kufuatilia sakata hilo, Amani lilinyetishiwa kwamba Kajala baada
ya kushindwa kuvumilia, ameamua kumshitaki mahakamani mama
Wema.
Chanzo chetu kinadai kuwa Kajala alifikia uamuzi huo baada ya
kushauriwa na familia sanjari na wafuasi wake (Timu Kajala) ambapo
sasa, timu hiyo na Timu Wema wameingia vitani tena.
“Kajala ameshawasiliana na wanasheria wawili na kutoa maelezo yake,
wao wanaandaa faili ili mashitaka yafike mahakamani, amekasirika
sana.“Amesema mama Wema ametumia nafasi ya kukutana na watu
kumdhalilisha bila kumpa nafasi ya kujitetea, ameona si sawa hata
kidogo,” kilisema chanzo hicho ambacho ni jirani na Kajala.

Katika sauti, mama Wema anasikika akitamka matusi (hayaandikiki
gazetini) huku Wema naye anasikika akimsihi mama yake asimtaje
jina Kajala kwa kuwa kufanya hivyo ni kumpaisha. Hapa inamaanisha
kwamba, Wema alitaka mama yake afunguke lakini bila kutamka jina
la mtu.
AGUNDUA TIMU KAJALA IMO NDANI YA BETHIDEI
Katika hatua nyingine, mama Wema alisema kauli iliyoashiria kwamba
Timu Kajala ilikuwemo ndani ya bethidei ya mwanaye. “Nasema haya
huku najua humu ndani kuna Timu Kajala, lakini nasema….(matusi
mazito)”
KAJALA SASA
Baada ya madai hayo yote, juzi, Amani lilimsaka Kajala kwa njia ya
simu ili kumuuliza ukweli wa madai hayo. Licha ya kutopokea simu ya
paparazi wetu, alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno ‘SMS’ na kuulizwa
kila kitu.
Hata hivyo, badala ya kujibu alikaa kimya, baada ya dakika kama
kumi na tano alimrushia kwa simu mwandishi wetu video hiyo ambayo
anadai kutukanwa na mama Wema bila kusema chochote hali
iliyotafsiriwa kuwa kama alisema; ‘hebu oneni wenyewe jamani,
nimemkosea nini mama Wema?
ALICHOKIFANYA MARTIN KADINDA
Katika hatua nyingine siku hiyo, meneja wa Wema, Martin Kadinda
alikuwa na kazi ya ziada kuhakikisha, mama Wema na mama
Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ hawakai jirani au meza moja licha ya
kwamba watoto wao wamependana.
“Kadinda ana kazi ngumu sana, unajua anatakiwa kuhakikisha kwamba
mama Wema na mama Diamond hawakai meza moja. Sijui anaogopa
nini, kwani hawa si watu ambao watoto wao wana mpango wa
kuoana?” alihoji mwalikwa mmoja.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Katika bethidei hiyo, Wema alizawadiwa magari mawili, Nissan Murano
lenye thamani ya shilingi milioni 36 alilopewa na Diamond na BMW 545i
lenye thamani ya shilingi milioni 56, inadaiwa alizawadiwa na Kadinda!

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni