Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Thursday, October 2, 2014



STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka ameanika ukweli kuhusu uhusiano
wake na aliyekuwa mchumba wake Malick Bandawe baada ya
kuwagundua wanawake wawili aliozaa nao mbali na yeye.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Rose aliamua kufungasha virago vyake
na kurudi kwa mama yake mzazi maeneo ya Kigogo baada ya
kugundua kwamba mchumba’ake huyo alizaa na wanawake wawili
tofauti na yeye ambaye ni wa tatu.
“Alichokizungumza Malick kwamba alishamuweka chini Rose na
kuzungumza naye si kweli, ila yeye Rose aliamua kurudi kwao baada
ya kugundua jamaa ana wanawake wawili aliozaa nao kabla yake,”
kilisema chanzo hicho.
Akaongeza: “Kile kilichosemwa na Malick kuwa anasikitika kuona
mtoto wake anakwenda kulelewa na mwanaume mwingine ni kujitetea
tu lakini ukweli ni kwamba mwanaye analelewa na yeye mwenyewe
kwa sababu yuko nyumbani kwa mama yeke.”
Juzi, paparazi wetu alimtafuta Rose kwa njia ya simu yake ya mkononi,
alipopatikana na kusomewa madai hayo alikata simu huku akisikika
akisema hayuko tayari kufunguka lolote kwa sasa.
GPL

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni