Ni roho mkononi. Hayo ndiyo maneno matatu yanayofaa kuelezea hali
ilivyo jijini Dar es Salaam na maeneo kadhaa nchini kwa sasa, hasa
pale mtu anapobeba fedha nyingi.
Matukio ya ujambazi kwa kutumia silaha yamekuwa sugu na
kusababisha wananchi wanaopeleka au kutoa fedha benki kuvamiwa,
kujeruhiwa au kuuawa mchana kweupe na majambazi wanaotumia
pikipiki.
Wananchi wamekuwa wakihoji ni kwa jinsi gani majambazi hao hupatataarifa za mtu aliyekwenda benki ama kuweka au kuchukua fedha.
Mkazi wa Tabata Kimanga, Dar es Salaam, Salum Mashati alisema:
“Haiingii akilini, utasikia mtu kaporwa fedha akitoka benki. Eti
majambazi wanasema kabisa toa hizo milioni 20, wanajuaje kuwa una
kiwango hicho? Huenda watu wa benki wanashiriki uhalifu huu.”
Hata hivyo, meneja wa tawi moja la benki lililopo Mlimani City,
ambaye hakupenda jina lake litajwe alikanusha madai hayo... “Si kweli
kwamba benki zinashirikiana na majambazi kufanya uhalifu huu.
Kwanza wahudumu (bank tellers) hawaruhusiwi kuingia na simu
wanapohudumia wateja.
Nini Kifanyike?
0 comments:
Post a Comment