Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale, anaamini kuwa fujo kwenye
show ya msanii wake huyo jijini Stuttgart nchini Ujerumani ilipangwa
itokee.
“Sisi tumefanya kazi na promoter wa Nigeria, wao wenyewe kwanza ile
advertize wakati wanamfuata Diamond hotelini hawakuwa wanaongea
vizuri,” Tale ameiambia Bongo5. “Mmoja ni Mnaigeria mmoja sijui niMsenegali.Ilikuwa imepangwa tu itokee, sometime vitu vingine
vinapangwa tu ili vitokee, yaani kwa sababu, sio tumepanga itokee,
imepangwa itokee, vitu vingine vinatokea for a reason,” ameongeza.
Kama isingekuwa polisi wa Ujerumani leo tungekuwa tunaongea habari
nyingine kwakuwa Diamond Platnumz aliponea chupuchupu
kushambuliwa na mashabiki wenye hasira jijini Stuttgart nchini humo
baada ya kuingia ukumbini saa 10 Alfajiri wakati mashabiki hao
walikuwa wakimsubiri tangaa saa 4 usiku.
Show hiyo ilikuwa ifanyike usiku wa kuamkia Jumapili.
Katika tukio hilo lililoandikwa na vyombo vya habari vya nchini
Ujerumani, promota wa show hiyo ambaye ni Mnaijeria alikimbia eneo
la tukio na DJ wa show kupewa kipondo cha paka mwizi.
Story kutoka Ujerumani inasema:
Majira ya saa 10 alfajiri Mwanamuziki nyota wa Bongo Flava Nasib
Abdul aka Diamond Platnumz alijukuta katika hali ya hatari hadi
kuokolewa na polisi mjini Stuttgart,Ujerumani,baada ya mashabiki
waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show. Mashabiki hao waliokuwa
wamelipa tiketi kwa Euro 25 kama kiingilio waliahidiwa kuwa show
ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijikuta wakisubiri hadi majira ya saa
10 alfajiri ndipo Diamond alipopelekwa jukwaani na promota wake raia
wa Nigeria anajiita kama Britts Event.
Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza
kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na
promota wake. Kilichowakera zaid mashabiki ni pamoja na vyombo
vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya
washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki ma-Djs walishambuliwa na
wapo Hospitalini kwa sasa.
Moja wa Djs hao alipoteza Laptop yake ,mwanadada DJ Flor alipatwa
mshtuko wa moyo na kukimbizwa hosptali. Mashabiki hao walimpa
kipigo DJ Drazee naye yupo hoi hospatali. Polisi nchini Ujerumani
wanamesema tukio hilo la aibu halijawahi kutokea,kuwa msanii
kuchelewa kufika jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari kwani
mashabiki wa Ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na
wamesema kuwa wanachunguza thamani ya hasara iliyosababishwa na
ghasia hizo na pia itamfungulia mashtaka promoter huyo raia wa
Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha namtandao fulani wa biashara.
Kupitia Instagram Diamond alidai kusikitishwa na tukio hilo.
Kiukweli nimesikitishwa sana na uandaaji wa kampuni hii ya BRITTS
EVENTS iliyoandaa show ya Stuttgart Germany… kinachoniuma na
kunisikitisha zaidi ni jins watu walivyoamua kujitolea kuja kwa wingi
kutusupport vijana wao, halaf mwisho wa siku promoter anatupeleka
wasanii kwenye show saa kumi alfajiri… najua ni kiasi gani mmeumia
na kuwa disappointed… lakini naomba mtambue kuwa halikuwa ni kosa
langu, coz mimi ni mgeni tu, na nafata maelekezo ya promoter…hivyo
nisingeweza kujiamulia kuja muda ninaoutaka mimi….
0 comments:
Post a Comment