Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Tuesday, September 2, 2014


Martin Kadinda ambaye ni meneja wa Wema Sepetu ameibuka na kusema kuwa Wema Sepetu
aliyekuwa akimwaga pesa vilivyo kwasasa hana pesa ya kumlipa bali yeye Martin anahangaika kwaissue zake binafsi ili wasilale njaa…
Kadina amesema kuwa yeye na Wema hawana mkataba wa kulipana bali wapo kishkaji zaidi.
“Wema hana pesa ya kunilipa mimi, ninachokifanya ni kuhangaika kutafuta deals ili mimi na yeye
maishani tusilale njaa, maisha ni kutegemeana.
“Kikubwa ninachofanya ni kutafuta dili za kazi nyingi ili tuweze kupeana pasu kwa pasu lakini si
mshahara, nafanya kazi na bosi wangu Wema kishikaji na kwa kweli nafurahia sana utaratibu huu”
Martin alisema kuwa kama angekuwa na mkataba na Wema kumlipa kila mwezi asingemudu na
kusema yupo na Wema kwasababu anajua ni mtu wa aina gani na anafanya kazi zake kwa uhuru bila
kubanwa
Wakati Wema yupo kimapenzi na yule kigogo aliyejulikana kwa jina la Clement(CK), Wema alidaiwa
kumwaga pesa kila kona na wapambe kibao wa kula bata nao huku akiwa na magari kadhaa lakini
kwasasa anadaiwa kushuka kiuchumi na kubaki na gari moja pekee huku wapambe aliokuwa nao
wakitimua na waliobaki kulalamika hawali bata kama zamani.
Hivi karibuni tena Diamond Platnumz aliye mpenzi wa Wema alisema kuwa Wema ni mtu wa starehe
na kuendekeza mashoga wapenda anasa badala ya kutumia fursa na umaarufu mkubwa alionao sasa
kufanya kazi zake kwa bidii hususani filamu

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni