Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Friday, September 19, 2014

UGONJWA MPYA WAIBUKA FACEBOOK

Watumiaji wa mtandao wa jamii
wa Facebook wameonywa juu ya
kuibuka kwa ugonjwa mpya wa ulevi wa
mtandao huo. Ugonjwa huo mpya
unajulikana kitaalamu kama Facebook
Addiction
Disorder (FAD).
Mtaalamu wa saikolojia Dr. Michael Fenichel,
ambaye ametoa machapisho kadhaa kuhusu
FAD mtandaoni, ameelezea dalili za ugonjwa
huo ni pale mtumiaji anapoipa kipaumbele
Facebook kuliko shughuli zingine za kila
siku kama kuamka, kula, kutumia simu
kwa matumizi mengine ama kusoma barua
pepe zingine.
"Jambo la kustaabisha ni kuwa, kama ilivyo
kwa simu za mikononi, hakuna mtu
anayegundua juu ya muda na
nguvu inayopotea kazini na majumbani.
Sasa hata watu watembeapo,
wamejitolea muda wao kwa ajili ya
Facebook.” Dr. Fenichel aliyazungumza hayo
katika chapisho la mtandaoni juu
ya changamoto mpya kutokana na FAD.
FAD inaweza pia kuelezwa kama
ulevi kupindukia wa tarakilishi. Jitambue
kuwa na ugonjwa huo endapo...
Kwa mujibu wa Joanna Lipari, mtaalamu wa
saikolojia ya tiba kutoka Chuo Kikuu cha
California, Los Angeles alipohojiwa na CNN
report, hizi ni dalili kama unaugua ugonjwa
wa FAD
1. Unapoteza usingizi kwa ajili ya Facebook.
Matumizi ya Facebook yanapokuwa ya lazima
kwako kiasi cha
kuwa logged in usiku kucha, matokeo yake
ni kushinda mchovu siku nzima ifuatayo.
2. Unatumia zaidi ya saa moja
ukiwa Facebook. Lipari alisema ni
vigumu kusema ni kiasi gani kiasi kikubwa
cha
matumizi ya Facebook, lakini kwa wastani
mtu anapaswa kutumia chini ya nusu saa
kwa siku akiwa Facebook.
3. Unaanza kuzoweana na kuwa karibu na
wapenzi wako wa zamani uliokutana nao
Facebook.
4. Unadharau kazi kwa ajili ya Facebook. Hii
inamaanisha unautumia muda mwingi
Facebook kuliko kutimiza
majukumu yako ya kazi..
5. Mawazo juu ya Facebook
yanakuacha katika wahka. Ikitokea
ukaikosa Facebook unapatwa na mfadhaiko,
wasiwasi ama dukuduku. Hii
inaashiria unahitaji msaada wa haraka
sana. Wataalamu wa tiba huko Marekani
wamekutana na ongezeko la
wagonjwa wanaokabiliwa na athari za
mitandao ya jamii, ikiwa ni pamoja na
kutofanya kazi ama kukosa hamu ya
mapenzi.
Facebook
Facebook, iliyoanzishwa na bilionea mdogo
zaidi ulimwenguni Mark Zuckerberg, ina
watumiaji zaidi ya
milioni 500 kote ulimwenguni, nusu
yao huingia Facebook kila siku. Idadi
ambayo kama ingekuwa ni nchi, basi
ingekuwa ya tatu duniani kwa idadi ya watu
baada ya China na India. Kuna picha zaidi ya
bilioni 2, huku video
zikiwa zaidi ya milioni 14 katika
kurasa mbalimbali za Facebook.
Takribani sekunde zipatazo bilioni 6
hutumiwa ndani ya Facebook kila siku,
kote ulimwenguni. Kwa mujibu wa Willis
Wee, mwanzilishi wa blog ya habari za jamii
na masoko ya Penn-Olson.com, idadi hii ni
zaidi ya
mara mbili ya idadi ya watumiaji
wa mtandao maarufu wa utafutaji wa Google

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni