Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Friday, September 19, 2014

Amri Kumi za facebook

AMRI YA 1
Usi-comment kwenye status ama picha
iliyowekwa mwezi uliopita. Kufanya hivyo ni
kuonesha unafuatilia maisha ya mtu kimya
kimya.
AMRI YA 2
Usi-like picha 3 mfululizo kwenye wall ya mtu
mmoja. Ni ishara kuwa unayachunguza mambo
yake kimya kimya.
AMRI YA 3
Usi-comment jambo ambalo ni nje ya topic ya
post husika. Kama mtu akiposti kuhusu
ng'ombe wewe usi-comment kuhusu mbuzi.
Bakia kwenye hoja husika.
AMRI YA 4
Usiandike status nusu nusu. Kwa mfano;
usiandike 'mwenzenu nina matatizo' Wajua fika
tutakuuliza una tatizo gani. Tuokolee muda
wetu kwa kuandika maelezo yaliyotosha kuwa
una matatizo baada ya kufumaniwa na mwenza
wako.
AMRI YA 5
Kutokana na amri ya 4, kama hupo tayri
kutuambia nini kilichokusibu ni marufuku
kumwambia mtu kwenye comment kuwa
unamu-inbox kumweleza matatizo yako.
AMRI YA 6
Usithubutu wala kujaribu wala kudiriki kum-tag
mtu picha ambayo yeye hayumo wala
hajakuomba ufanye hivyo.
AMRI YA 7
Kwa wanawake, kama utaamua kupiga picha
bafuni ili uipost facebook hakikisha
unakumbuka kuvaa kufuli lako.
AMRI YA 8
Kwa wanaume, kama msichana ata-like ama
ku-comment kwenye status ama picha yako
haina maana anataka umtumie inbox.
AMRI YA 9
Kwa wanawake, kama mwanaume atakutumia
friend request haina maana anakupenda ama
anakusudia kukutongoza.
AMRI YA 10
Kwa wanaume, kama msichana ata-accept
friend request yako, haina maana ukimtongoza
atakukubalia kirahisi.
MWISHO WA AMRI
Imetupasa kuitumia facebook kwa matumizi
mazuri na yenye tija. Ole wao wanaopoteza
muda wao facebook kutafuta wanawake ama
wanaume. Watu hao watajikuta hawajafanya
lolote la maana maishani na kuanza kuwaonea
gere wenzao waliofanya kweli.
Ukigombana na mpenzi wako usije kutuambia
facebook kwa kuwa hata mnaposigina amri
huwa hamtushirikishi.
MWISHO.

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni