Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Friday, September 19, 2014

DALILI 20 ZA MWANAMKE ASIYEKUPENDA KWA DHATI!

Dalili 20 za mwanamke asiyekupenda kwa
dhati!
1 : Hataki kuambata na wewe katika
matembezi na ikitokea anakuwa mtu wa
masharti mara akuambie tangulia nakuja
au pengine kutembea nawe kwa umbali.
2 : Anapata kigugumizi kukutambulisha
kwa rafiki zake na ndugu na inapotokea
amebanwa hafikishi ujumbe kwa kiwango
timilifu.
3 : Haoneshi kubana matumizi kwa ajili ya
maendeleao, kwake ni kufuja mali na
anapokosa kupewa pesa ni mwepesi
kulalamika na wakati mwingine kununa
kabisa.
4 : Anaahilisha mara kwa mara kukutana
na wewe tena bila kukueleza sababu za
msingi Au kukutungia uongo wa dhahili na
kuusisitiza bila kuona aibu.
5 : Anapokuwa akitoa maelezo ya
mwanaume amtakaye sifa zake zinakuwa
hayalingani na wewe. Anaweza kukuambia
napenda kuishi na mwanaume mwenye
gari au mwenye mwili mkubwa, sifa
ambazo wewe huna!
6 : Hacheki kwa furaha hata kama
ukimchekesha haoneshi furaha ya moyoni.
Tena mara nyingine anakuwa mkimya na
mshiwishi mkubwa wa kuachana kutoka
kwenye matembezi yenu ya jioni. “Aaah,
mi nimechoka narudi nyumbani”
7 : Anajaribu kukuunganisha na
wanawake wengine na haoni vibaya
anaposikia unamfukuzia mwingine badala
yake anakutia moyo wa kuendelea na
usaliti wako. Hana wivu kabisa.
8 : Hajuti anapokukosea, mwepesi wa
kujitenga, kutokuzungumza nawe na
mwingi wa kukusukumia makosa hata
kama yeye ndiye aliyekukosea.
9 : Msambazaji wa habari za udhaifu wako
na mtu asiyekusifia mbele za wenzake. Si
balozi mwema kwa familia yake, haishi
kukuponda mbele ya wazazi na ndugu
zake.
10 : Mwepesi wa kupokea na si wa kutoa
mmiliki wa mali zako na mkumbatiaji wa
mali zake pia. Msiri wa mipango yake na
mtu anayependa kujua zaidi ya kwako
kuliko wewe kujua yake.
11: Hathamini uwepo wako na
anakuchukulia kama mtu wa akiba.
Hakumis unapokuwa haupo,
hahisi upweke wala hakukumbuki
unapokuwa mbali naye.
12 : Hakutii moyo unaposhindwa na mara
nyingine hauzuniki nawe unapokuwa una
shida,. Hachukui huzuni yako kama yake,
hakufariji na hakusaidii kutatua
kilichokwama.
13 : Mhamasishaji wa uasi hasa wa watoto
na ndugu, anayeweza kuchochea hisia za
jamii ikuone mbaya, ukudharau na wakati
mwingine ikutenge. Mwenezaji wa sifa
zako mbaya.
14 : Hakupi kipaumbele katika maamuzi,
anajiona yeye ndiye wa kwanza na wewe
ni mtu wa kufuata hata unapopinga
hasitishi dhamira yake ya kutenda.
15 : Humsisimui katika mambo ya faragha,
anakuchukulia kama ndugu yake.
16 : Hakuhudumii tendo la ndoa mpaka
siku amependa mwenyewe. Ni mwingi wa
sababu za kuchoka kusingizia ugonjwa na
mwenye kuhisi kero ya kucheza nawe
mchezo wa kikubwa.
17 : Hazungumzii maendeleo yenu,
mwepesi wa kushawishi ilivyopatikana
viuzwe ili atimize hitaji lake. “Niuze simu
yangu niende kuwaona wazazi, maana
kuna sherehe ya motto huko!”
18 : Hataki kuambiwa ukweli na
anapotokea akaambiwa anajitetea kwa
kumtaja mwanaume mwingine. “Mbona
Shabani (si jina halisi) anamfanyia hili,
hamfanyii hivi mkewe”
19 : Hasamehe na kusahau. Kosa la
mwaka juzi analijengea hoja.
20 : Mwepesi wa kutoa kauli za kutengana
na asiyeogopa kuachwa. “Kama vipi kila
mtu akae kivyake maana naona unaniboa
tu, unadhani nitashindwa kuishi bila
wewe”

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni