Niliamka mapema na kujiandaa kwenda kazini kwangu.
Lakini nilipofika kazini siku ile nikajiona sio mtu wa kawaida kwani kila mtu aliniuliza Maswali mengi yasiyo na kawaida.
Mara mbona leo hauko smart kama kawaida yako na wakati nataka kumjibu huyu jamaa, mara akaja Habiba binti ambaye ni secretary wangu na kunipa perfume na kusema, "Boss leo haukulala nyumbani au weekend ulilala nyumba ndogo??"
Ile hali ikaniboa sana nikaingia ofisini kwangu na kujifungia, nikaanza kukumbuka ugomvi wangu na mke wangu uliotokea ijumaa.
Kisa cha ugomvi ni baada ya kuniuliza kwa nini nimechelewa kurudi, nikamsukuma na kumpa vibao kadhaa kabla ya kumpigia dereva na kumwambia awahi asubuhi kuwapeleaka stand na kisha waende kwa mama na baba kijijini.
Weekend ile kwa kuwa hakukuwa na mtu nyumbani mie nilikula hotelini na nikiwa nabadilisha wanawake kama mashati huku nikichezea fedha kama sina akili nzuri.
Na mke wangu pamoja na yote alikuwa akiniudhi pale anaponikumbusha kumtumia baba na mama baadhi ya mahitaji na kwa kuwa niliona haina mpango nikawa nikiona kama ananizingua tuu.
Nikiwa naendelea kuwaza pale ofisni nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni msamaria mwema na kudai kuwa walikuwa wako katika basi dogo, wakiwa wanatoka kijijini kwetu kwenda mjini mama na baba walipatwa homa ya ghafla wote wawili kwa hiyo mke wangu akawa akiwasindikiza hospital na kwa bahati mbaya wamepatwa na ajali mbaya na wote wamefariki pale pale.
Nikiwa nimesimama pale kwenye kiti na akili ikiwa imesimama kwa hofu mara akanipigia simu na mdogo wangu aishie kijijini na kusema mwanangu wa kwanza na wa pekee aliposikia mama yake, bibi na babu wamekufa akatoka nyumbani akiwa hajitambui huku anakimbia hovyo na kagongwa na bodaboda na kavunjika miguu yote miwili na mikono kakimbizwa hospitalini hviyo wanahitaji masada wa fedha za mazishi na mtoto.
Jasho likaanza kunitoka nami bila kumuaga mtu pale ofisini nikatoka na kulichukua gari langu huku nawahi nyumbani nikiwa nakaribia kuingia barabara ya mtaa wa nyumbani kuna dereva wa bajaji akaingia upande wangu na nikamgonga na kumuua pale pale.
Baada ya kuona kelele za wananchi wenye hasira kali wakija ikanibidi nikimbie na gari na nikiwa natoka spidi nigamgonga ubavuni kijana mmoja na sikuangalia kama alipona au lah.
Nikafanikiwa kufika nyumbani na kubadili gari na kuondoka nikielekea airport ili niukimbie mji maana nilihisi kwa jinsi wanavyolifahamu gari langu, polisi watakuwa wameshaanza kunisaka na ukizingatia kituo kipo jirani.
Njia rahisi na ya haraka pale ikawa ni kwa kutumia usafiri wa anga hivyo nikakimbia na kuliweka gari kwa rafiki yangu na kunikimbiza mpaka airport na kumwomba aende kijijini kusimamia mambo maana mie sasa hali yangu taabani.
Nikafanikiwa kufika airpot nikaingia kwa agent wa kampuni ya ndege anipe tiketi ya kwenda Mbeya ili nifanikiwe kukimbia kwenda tunduma na hatimaye kwenda zambia kukaa mafichoni.
Nikafanikiwa kupata ticketi na kusafiri mpaka Mbeya na kupanda magari ya kwenda tunduma mpaka ofisi za uhamiaji.
Nikiwa pale tunduma najianda kupata kibali cha muda cha kwenda Zambia nikawa nashangaa kuona watu wakinitazama sana nikaanza kuogopa na muda mchache polisi wa pale wakanidaka kumbe muda huo wote picha yangu ilishatolewa kwenye TV kuwa natafutwa kwa kusababisha ajali na kuua watu wawili na nimetoroka.
Wakanidaka na nikaanza kulia pale na wao wakawa wanajiandaa kwenda kunipelekeka kituoni..............................................................................................................................Mimi nikawa naendelea kulia mpaka pale mama watoto aliponiamsha na kuniambia mbona umekuwa ukilia na ni usiku sasa unaumwa?
Kidogo nikimbie nikamuuliza kumbe hujafa? Nikatoka mbio nikaenda chumba cha mwanangu na kumkuta yupo, nikanyanyua simu na kumpigia baba na mama pamoja na mdogo wangu na rafiki yangu usiku ule nikawaambia nawapenda na kufurahi kuwa bado wazima.
Ndoto hii amini usiamini imenifanya nizidishe mapenzi kwa mke, mtoto, baba, mama, kaka, wadogo na ndugu zangu wote.
Kwani niliwasahau sana na mapenzi kwa familia na kila mtu yalipungua, kumbe ndoto ni njia ya kutufanya tubadilike...
Nimeamini kwa muda mfupi tu dunia ilianza kuwa jehanamu
Nawapenda ndugu zangu... wewe je?
Share kwa kila unayemjali na mwambie unamjali
Soma zaidi hapa

0 comments:
Post a Comment