Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Wednesday, September 17, 2014

Leo Katika Historia



Tarehe 17 Septemba miaka 32 iliyopita, Mafalanja wa Lebanon wakishirikiana na askari wa utawala haramu wa Israel walifanya mauaji makubwa katika kambi za wakimbizi wa Kipalestina huko Sabra na Shatila nchini Lebanon. Mwezi Juni mwaka 1982 askari 150,000 wa utawala haramu wa Israel waliishambulia ardhi ya Lebanon na baada ya kuwalazimisha wapiganaji wa Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) kuondoka Beirut na kuukalia mji huo kwa mabavu. Menachem Begin Waziri Mkuu wa wakati huo wa Israel na Ariel Sharon Waziri wa Vita wa utawala huo, tarehe kama ya leo waliliamuru jeshi la Israel kuzizingira kambi za Sabra na Shatila na kisha Mafalanja wa Lebanon wakaanza kufanya mauaji ya umati dhidi ya wakimbizi wa Kipalestina waliokuwa katika katika kambi hizo. Wapalestina 3,300 waliuawa shahidi katika mashambulio hayo.
Tarehe 26 Shahrivar miaka 34 iliyopita kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Shamsia, utawala wa zamani wa Iraq ulifuta kwa upande mmoja makubaliano ya mipaka ya mwaka 1975 yaliyojulikana kwa jina la Mkataba wa Algeria kati yake na Iran. Siku hiyo, Saddam Hussein kiongozi wa zamani wa Iraq aliuchana mkataba huo wa Algeria mbele ya kamera za televisheni akiungwa mkono na madola ya kibeberu katika. Siku kadhaa baadaye, Saddam Hussein alianzisha uvamizi wa miaka minane dhidi ya ardhi ya Iran.
Na siku kama ya leo miaka 748 iliyopita alifariki dunia Ibn Nafis msomi na tabibu wa Kiislamu aliyevumbua namna damu inavyozunguka kwenye mapafu. Alianza kujifunza masomo ya dini ya Kiislamu akiwa katika mji alikozaliwa wa Damascus na akafunzwa pia sayansi ya tiba na walimu mashuhuri wa zama hizo. Ibn Nafis alipata maarifa makubwa baada ya kufanya utafiti wa kina. Mojawapo ya vitabu mashuhuri vya Ibn Nafis ni kile alichokipa jina la" Muujaz al Qanun (The Summary of Law) ambacho kinaelezea vyema namna damu ya mwili inavyozunguka. Ibn Nafis alikuwa tayari amevumbua mzunguko huo wa damu karne tatu kabla ya raia wa Ulaya, Miguel Serveto kubainisha kwa usahihi kuhusu mzunguko huo wa damu katika mapafu. Al Shamil fi al Tibb ni kitabu kingine cha msomi huyo wa Kiislamu kilichokusanya mjadala mpana kuhusu mbinu za upasuaji.

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni