Tunaendelea na Exclusive Interview ya mwigizaji ambaye amepitia mitihani mizito maishani mwake, Wastara Juma. Hakukata tamaa, anaendelea kudunda hadi leo.
Wiki iliyopita tuliishia hapa:
“Baada ya kuwa na ujauzito wazazi wangu waliamua kunichukua nikaenda kukaa nao Zanzibar lakini nikawa nateseka sana ambapo mama yangu aligundua na kusema nije Dar kwani anataka kuniona na kipindi hicho alikuwa anaumwa, nilikuja kwa mama aliponiona alihuzunika sana kwani nilikuwa nimedhoofika.
SASA ENDELEA…

AUZA GENGE
Licha ya kudhoofika mwili lakini pia wakati huo nilikuwa na mimba ya miezi mitano.
Mwandishi: Baada ya kumuona mama yako nini kiliendelea?

“Nilienda kwenye chumba tulichokuwa tukiishi na mume wangu maeneo ya Tabata nikakuta kodi ilishaisha na mume wangu hana hela ya kulipia kwani baada ya kunioa familia haikushughulika tena kumlipia kodi,
alipoona mambo magumu hivyo alinirudisha kwa mama yangu na vitu vyetu vya ndani akamuomba akae na mimi huku akimuomba msingi wa kufanya biashara ambapo mama yangu alimpa.
“Baada kupewa msingi tulifungua genge lakini baada ya wiki mbili aliaga kwamba anaenda nyumbani kwao Zanzibar na kuniacha nikiendelea na biashara ya genge baadaye nikafungua ‘cafe’ huku nikiwa nyumbani kwa mama yangu nakumbuka hata siku nikiwa naumwa uchungu nilikuwa nakaanga maandazi ya biashara.
MUME ATOWEKA MUDA MREFU
Mwandishi: Mumeo alirudi baada ya muda gani?
“Ukweli ni kwamba tangu aliponiacha nikiwa na mimba ya miezi mitano alirudi siku nikiwa leba najifungua, nilijifungua mtoto wa kiume ambapo hapo ndipo mat atizo yalizidi kwani hakuwa akitoa matumizi ya mtoto, alirudi kwao Zanzibar na hakuwa akiwasiliana na mimi wala nini.

AKOMBWA VYOMBO VYA NDANI
“Kilichoniuma zaidi ni kwamba mwanangu akiwa mchanga ndugu zake walikuja nyumbani na kuchukua kila kitu mpaka magodoro na kusema walinunua wao hivyo nikawa sina pa kulala na mwanangu hivyo ikanibidi nimtafute na kumwelezea ambapo aliniambia nimfuate nyumbani kwao Zanzibar tukazungumze zaidi.
Mwandishi: Nini kiliendelea, ulienda Zanzibar?
“Nilienda. Nilimuacha mwanangu nikawahi asubuhi ili jioni nirudi huku ndugu zangu wakinipa fedha kama laki moja za kuwanunulia watoto vitu vya shule, nilipofika huko niliwakuta na ndugu zake tukafanya kikao ndipo nikawaeleza kwamba nina shida na fedha kwa ajili ya matumizi ya mtoto na hela ya kununua godoro lakini wakaniambia kwamba hawana hela na hali yao ni mbaya kimaisha.

MUME AMPORA POCHI
“Ilipofika saa tisa niliaga ambapo mama mkwe wangu alinipa shilingi mia tano nikamuuliza ya nini akaniambia hana nyingine, walinisindikiza lakini cha kushangaza tulipofika mbele kidogo mume wangu alinipora pochi iliyokuwa na fedha za kununulia vifaa vya shule vya watoto nilivyoagizwa na ndugu zangu.

“Nilimkimbiza na kumnyang’anya lakini alikuwa ameshachukua hela zote ambapo tulianza kupigana nikamshika sehemu za siri akaishiwa nguvu hapo nikaweza kupenyeza mkono kwenye mifuko yake ya suruali na kuzichukua huku nikikutana na mahirizi kibao hivyo baada ya hapo tukawa tunatukanana huku na huku baada ya kumwachia naye akawa anamkimbiza.
POLISI WAMUOKOA
“Bahati nzuri tulikutana na difenda la polisi na hiace ikiwa mbele yake wale polisi walishuka na kuuliza kulikoni hapo ndugu zake wakamtetea wakiwaambia polisi kwamba ni mgonjwa wa akili, nikapata upenyo nikaingia kwenye hiyo hiace yaani nililia mpaka nilivyoshuka stendi na tangu siku hiyo nikamchukia sana huyo mwanaume.

0 comments:
Post a Comment