Stori: Musa Mateja, Kahama
MTANGAZAJI wa Clouds FM, Fatuma Hassan ‘DJ Fetty’ na DJ Muli B, wamenaswa wakiwa kwenye pozi la mahaba huku tena wakiwa wamejisahau utadhani mume na mkewe.
MTANGAZAJI wa Clouds FM, Fatuma Hassan ‘DJ Fetty’ na DJ Muli B, wamenaswa wakiwa kwenye pozi la mahaba huku tena wakiwa wamejisahau utadhani mume na mkewe.
Ishu hiyo ilitokea Agosti 17, Mwaka huu ndani ya Uwanja wa Kahama, ambapo walienda kwa ajili ya kutazama burudani za Serengeti Fiesta 2014 zilizokuwa zikifanyika siku hiyo.
Wakiwa nyuma ya jukwaa, wawili hao walionekana kubebana wakati wamekaa jambo lililowafanya baadhi ya wasanii waliokuwa nyuma yao kukonyezana na wengine kuulizana maswali ambayo hayakuwa na majibu kama ni wapenzi au laa.
Paparazi wetu apowauliza kama wana uhusiano wowote, wawili hao walikanusha na kusema wamepozi kama mtu na mfanyakazi mwenzake Clouds FM
0 comments:
Post a Comment