Tunaendelea na mada yetu ya maswali 10 ya kujiuliza kabla ya kuachana (talaka). Tumalizie makala haya tuliyoyanza wiki nane zilizopita:
Inapotokea kweli ulimkosea na uliomba msamaha na ukajirekebisha lakini bado mwenzi wako ana kinyongo, hakikisha unafanyia kazi hili suala. Vilevile kama ni wewe ndiye unashindwa kusamehe, tuliza akili na upitishe msamaha wako.
Kwa mantiki hiyo, kabla ya kusimamia uamuzi wa kuachana, tafadhali sana pitia matukio yenu ya nyuma. Sahihisha pale ulipomkosea, samehe alipokukosea, sawazisha palipo na kinyongo. Inawezekana mkawa na maisha mazuri zaidi kwa kuvumiliana kuliko kuachana.
9. MNA WATOTO, NAFASI YAO IPO WAPI?
Hili pia ni la maana sana kwako. Mwenzio anapokuudhi lazima ujue haki zake pia, sio kuamua vile unavyojisikia. Inapotokea kwamba huyo unayetaka kuachana naye ni mama au baba wa watoto wako, umakini zaidi unahitajika.

Jiulize, baada ya kuachana watoto nafasi yao ipo wapi?
Tafsiri ya wawili kuachana ikiwa wana watoto ni ubinafsi, kwamba wewe na mwenzio mlitafakari nafasi zenu na hamkufiria nafasi ya watoto. Hakuna malezi yoyote bora ambayo yanawatenganisha watoto na wazazi wao. Kwa nini hisia zako usizirudishe nyuma ili watoto wako ‘wainjoi’ malezi ya baba na mama.

Hata hivyo, ni vizuri kutambua kuwa kabla ya wazo la kuachana kuna makosa yalifanywa. Kabla hujawa msumbufu kwenye ndoa yako, fikiria nafasi ya watoto wako. Mathalan; ukiwa unawapenda watoto wako lazima utakuwa unaipenda familia yako, maana furaha ya wanao ni uwepo wa wazazi wao wote.
Kama wewe ni baba, ikiwa na unawapenda watoto wako, utahakikisha humtendi vibaya mama yao. Kadhalika kwa mama, kwa thamani ya watoto wake, lazima ahakikishe baba wanaye anakuwa vizuri siku zote, hivyo kujiweka mbali na misuguano kama siyo ugomvi.
Kwa hatua hiyo ya kujizuia na kujichunga, itumike hata baada ya kugombana. Ni kweli amekuudhi na unaona anastahili kuachwa, basi rekebisha uamuzi wako japo kwa kutafakari nafasi ya watoto. Zingatia kuwa kuachana kwenu, wanaoathirika zaidi ni watoto.
•BADO UNAHISIA NA MWENZI WAKO
Ukishajiuliza maswali yote, hili lifanye la mwisho. Watu wengi wameachana na wenzi wao kwa kuongozwa na hasira lakini ukweli ni kwamba ndani ya nafsi zao wanakuwa bado wana upendo mkubwa sana. Kwa nini umuache unayempenda?

Hata siku moja usije ukapuuza hisia zako, zina maana kubwa sana. Muunganiko (chemistry) ambao umejitengeneza kati yenu, si rahisi kutokea kwa mtu mwingine. Ukijidanganya na kuamini kuwa hali uliyonayo kwa mpenzi wa sasa, utaipata kwingine unafeli.
Kipengele hiki nimekiweka cha mwisho kwa sababu kina maana ya utetezi binafsi. Kama hutajitetea mwenyewe na hisia zako, usitegemee atatokea mwingine wa kukusaidia. Kwa vile unampenda sana mwenzio, ni vizuri ukachukua uamuzi wa kumuweka chini na kurekebisha kasoro iliyojitokeza kuliko kumwacha aende.
HITIMISHO
Katika pointi ya wazi na rahisi zaidi ni kuwa mtu huwa hang’ang’anizwi au kubembelezwa kuendelea na mwenzi wake. Isipokuwa hushauriwa kwa hoja ambazo humuingia mhusika na kuamua kubadili uamuzi. Kusamehe ni utashi wa mtu, maana yeye ndiye anayejua ubora na ubaya wa mtu.

Kusamehe ni ridhaa ya moyo kwa sababu kama umeshakinahi, hata ije mbeleko ipi, matokeo yake ni mabaya sana. Hutokea watu ugomvi mdogo kukumbushiana matukio mabaya yaliyopita. Hii husababishwa na kukosekana kwa msamaha wa kweli.
Yote kwa yote, ni vema kutambua kuwa inauma sana kuachana na mtu ambaye mwanzoni mlipendana. Anayeweza kutengana na mpenzi au mwanandoa mwenzake akiwa anatabasamu, huyo bila shaka atakuwa na ushawishi wa pembeni. Na kwa hakika, baadaye mtu wa aina hiyo hujuta sana yanapomrudia.
Somo letu linahusu maswali ya kujiuliza kabla ya kuchukua uamuzi wa kuachana au kupeana talaka (kwa wanandoa). Binadamu si kama mbuzi, kwa maana hiyo wanapokutana, kunakuwa na sababu ya kukutana kwao, hivyo haitakiwi kuamua kuachana bila angalizo.
Katika makala haya, bila shaka umejifunza au umejiongezea elimu kuhusu maswali 10 ambayo ama yanaweza kukufanya urudi nyuma na kuendelea kuujenga uhusiano wako au kushikilia msimamo wa kuachana lakini ukiwa na akili iliyo bora kabisa. Asante
0 comments:
Post a Comment