Mwimbaji wa Tip Top Connection, TundaMan aliwashangaza wengi baada ya
kueleza kuwa alipokea simu yenye namba nyingi asizozielewa na ghafla
akapata mshtuko na kuishiwa nguvu, hali iliyomsababisha akimbizwe hospitali
ambapo alipewa matibabu.
Licha ya kuwa wataalam na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)
walieleza wazi kuwa kitaalam simu haiwezi kabisa kuwa chanzo cha tatizo
hilo, TundaMan alisisitiza kuwa yeye ndiye aliyepata tatizo na anajua
kilichotokea.
“Wao wanasema haiwezekani kwa sababu hilo tatizo halikuwakuta…lakini
kwa kuwa mimi ndiye nimekuwa affected kwa siku mbili tatu, mimi naaminikuwa tukio hilo lipo na limekuja baada ya kupokea ile simu. Wao wanaongea
kitaalam siwezi kubishana nao, lakini mimi limenikuta na nimeona.” Aliiambia
tovuti ya Times Fm.
Kutokana na sintofahamu hiyo, Tundaman ameeleza kuwa msanii mwenzake,
Ali Kiba alimshauri kwenda katika nyumba ya ibada ili apate dua maalum.
“Yeah inawezekana (ni ushirikina) kwa sababu vitu kama hivyo huwa
vinatokea sana na ndio maana ndugu yangu Ali Kiba amenishauri nikapate
dua.” Amesema Tunda Man.
Ameeleza kuwa tayari amechukua uamuzi huo ingawa hali yake pia
inaendelea kuimarika baada ya kupata matibabu. Kwa mujibu wake, Dua
ndilo kimbilio lake la mwisho.
0 comments:
Post a Comment