Stori: Gladness Mallya
MWANADADA kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’
amepangua madai kuwa ni mjamzito na kudai ni maneno ya ya watu licha ya
kwamba ukikiangalia kwa makini kitumbo chake unaweza kuhisi kuna kitu
ndani.
Akizungumzia madai hayo na kwamba ndicho kinachomfanya asijichanganye
na wenzake kama kawaida, Nisha alisema kutoonekana kwake ni maamuzi tu.
“Eti nina mimba! Mh…nashangaa sana, sijui watu wanatoa wapi hayo
maneno, mimi sina mimba na nilikuwa sionekani kwa sababu nilisafiri, pia
mwezi mtukufu huwa sitoki hovyo, nikiamua kuzaa watu wataniona tu,”
alisema Nisha.
0 comments:
Post a Comment