STAA wa filamu Bongo, Baby Joseph Madaha amemwagana na aliyekuwa
mwandani wake ambaye pia ni meneja wake, Joe Kairuki pasipokuwa na
sababu za wazi.
Chanzo chetu cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina lake kimetutonya
kuwa, Madaha na Joe wamebaki kuwa mtu na bosi wake ila msanii huyo sasa
amejiweka kwa mwanaume mwingine.
Katika kujua ukweli wa ishu hiyo, mwandishi wetu alimpigia simu Madaha
ambaye alisema: “Hee unaniuliza kuhusu Joe, mbona umechelewa kujua?
Nimeachana naye, sasa nimejipatia mpenzi wangu mwingine na tunapendana
kupita maelezo.”
0 comments:
Post a Comment