Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Friday, August 8, 2014


Tumezoea kuona kwenye filamu au tamthilia simulizi la msichana mrembo
anaotoka katika familia ya kitajiri aliyechagua kuyaacha maisha ya raha na
kuishi uswahili na kijana anaempenda.
Huko Kenya, kumeripotiwa tukio halisi lililovuta hisia za wengi na
kuzungumzwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari,
ambapo msichana wa kihindi ameamua kuachana na familia yake tajiri na
kuambatana na kijana wa Kenya aliyezama nae kwenye vilindi vya mahaba.
Msichana huyo wa kihidi anaifahamika kwa jina la Sarika Patel, ameolewa na
kijana wa kabila la Bukusu, Timothy Khamala uamuzi ambao ni nadra
kutokana na mila na desturi za kihindi na kilichoshangaza zaidi ni kuwa wawili
hao wanaishi maisha duni kijijini.
Kwa Sarika, maisha ya umasikini sio kikwazo cha kulipata penzi la kijana
Timothy aliyenasa kwenye penzi lake.
Safari ya penzi la Sarika na Timothy ilianzia nyumbani kwao Sarika ambapo
kijana Timothy alikuwa akifanya kazi na baadae kutimuliwa kwa kudhaniwakuwa ana uhusiano na princess wa jengo hilo (Sirika) jambo ambalo lilikuwa
kweli.
Ingawa wawili hao wamejitoa na kuendelea kuishi pamoja licha kukiri kuwa
wanakabiriwa na changamoto kubwa ya kutengwa na jamii ya upande wa
familia ya kwao Sarika kwa kuwa kitendo hicho sio sahihi hata kidogo kwa
mujibu wa mila na desturi zao, ambapo watu wa jamii sawa ndio wanaooana.
Hata hivyo, Sarika ameelezea msimamo wake kuwa utofauti wa rangi na
tamaduni au ufukara wake hauwezi kumtenga na mpenzi wake wa dhati
Timothy.
Mapenzi sio pesa, mapenzi ni moyo

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni