Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Friday, August 8, 2014


Mkazi mmoja wa Kijiji cha Lundusi Kata ya
Peramiho wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma,Bibi
Scholastica Mhagama amesema miaka mingi
ameishi maisha dhiki na kunyanyaswa bila msaada
kutoka kwa jamii anayoishi hali ambayo imemfanya
amuombe Mungu amchukuwe ili azikwe kwenye
jeneza alilojiandalia.
Bibi Scholastica akiwa kwenye jeneza alilojiandalia
“Kila siku naomba Mwenyezi Mungu anichukue
haraka ili nikapumzike kutokana na mateso
ninayoyapata, lakini hofu yangu nikifa je, nitazikwa
kama binadamu wengine? Ndiyo maana nimeamua
kujitayarishia jeneza langu,” anasema Scholastica
Mhagama (76) mwenye ulemavu wa viungo
anayeishi pekee yake katika kibanda kilichoezekwa
kwa nyasi.
“Nimetengeneza kabisa jeneza langu siku nikifa
wanizike humu. Naomba Mungu anichukue haraka
ili kuepukana na mateso haya. Nimetengwa na jamii
na majirani wanashindwa kunisaidia wanadai eti
mimi ni mchawi kwa sababu watoto wangu wote
wanne walikufa wakiwa wadogo. Naumia sana
kusingiziwa kitu ambacho sikijui,’’ anasema kwa
masikitiko.
Bibi huyo anasema kuwa aliweza kutengeza jeneza
hilo baada ya kupewa Sh40,000 na mfadhili mmoja.
“Tayari nilikuwa na mbao kwangu, hivyo kazi ilikuwa
kumlipa kijana fedha na kumpa mbao ili
anitengenezee jeneza,” anasema.
Source:Mwananchi
- See more at: http://mwanaharakatimzalendo.blogspot.com/2014/08/bibi-wa-mjini-songea-ajitengenezea.html#.U-SaEKjogYo

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni