Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Thursday, August 7, 2014

Mambo ya ajabu ajabu usiyoyajua kuhusu binadamu


Wakati wewe unatoa mimba, kuna mtu anasaka mimba kwa miaka kumi bila mafanikio

Wakati wewe kijana una mkataa binti uliyempa mimba, kuna mzee ana miaka nenda rudi akiwa anakesha akiomba Mungu amjalie mtoto

Wakati wewe una inyanyasa familia yako leo, kumbuka kuna mtu anatamani apewe familia na aipende

Wakati wewe unaichukia kazi uliyonayo, kuna mtu ana vyeti vyake safi ila hajawahi kupata kazi ya aina yoyoye na anaishia kwenye interview tuu

Wakati wewe unawadharau na kuwasahau wazazi wako bila kuwajali. Kuna watu wanalia usiku kucha na kuumia kuwakosa wazazi

Kumbuka, hakuna maisha yoyote zaidi ya haya na huna budi kuwa na shukrani kwa kile unachojaliwa sasa.... Pia ni bora kuwa na mpangilio wa maisha ukimtanguliza MUNGU na kushukuru kila ulichonacho na kufurahia nyakati ulizonazo

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni