Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Thursday, August 7, 2014



Wapenzi wawili waliokuwa wamekaa kwa muda mrefu katika mahusiano yao ghafla wakajikuta wakianza kuandamwa na ugomvi wa mara kwa mara baina yao.

Binti kila alipokutana na marafiki zake walimpa maneno mengi juu ya mpenzi wake kuwa ana wanawake wengi na umbea wa kila aina. Na binti kila akirudi nyumbani daima ilikuwa ni ugomvi mkubwa na maelewano kupotea kwa siku kadhaa.

Na kwa upande wa kijana naye kila akikaaa kijiwezi alikuwa anaishiwa nguvu kuambiwa mara mkeo jana kashushwa na gari hapa,mara jana kaonekana hoteli fulani. Zile habari zikawa zinampa wakati mgumu na akirudi nyumbani ikawa ni ugomvi na majibizano ya ajabu.

Habari zikasambaa mpaka zikamfikia mzazi wa yule kijana na akawaita, walipofika akawaambia kwa nini mnagombana mara kwa mara? Kila mtu akamtupia lawama mwenzake, kuwa mara anasikia hivi mara vile.

Mzee kachukua lundo la fito zilizofungwa pamoja na kuwaambia wasaidiane kuzivunja. Wakajaribu kwa nguvu zote na kisha wakajikuta wakishindwa.

Mzee akampa kila mmoja fito moja na kumwambia aivunje, wote wakaweza kwa mara moja.

Mzee akawaambia kuwa sasa angalieni, " nimewapa lundo la fito na wote mkashirikiana kulivunja mkashindwa, na sasa nimewapa fito moja moja kila mtu mmefanikiwa kuzivunja. Laiti kama mngeshikamana kama lundo la fito hizo kamwe msingeyachukua maneno ya watu na kuyaamini, lakini kwa kuwa hamjashikamana basi watu wametumia mwanya huo kuwaumiza na kupoteza furaha yenu"

Mfano wa wapenzi hawa ni sawa na mahusiano mengi tuliyonayo sasa, watu tumekuwa wepesi wa kuamini maneno ya watu na kujikuta tukiwapoteza watu tulio wapenda au waliotupenda kwa dhati.

Funzo

Usipende kuamini watu wayasemayo kuhusu wewe na maisha yako na kama ukiyapata basi chukua kama changamoto na kujifunza zaidi na sio yakuharibie mambo yako

Usiwe mwepesi wa kuchukua maneno ya watu na kuyatolea hukumu kabla ya kuyafanyia uchunguzi.

Shikamana na umpendaye na kuamini yeye ni bora kuliko mwingine na daima ana upendo wa dhati juu yako.

Kujenga wasi wasi juu ya mwenzako ndio mwanzo wa kufarakana kwani hutampenda kwa dhati amini kila alipo yupo kwa jina la mapenzi yenu

MUHIMU: Kumbuka sio kila mtu anayekuombea mema katika mahusiano yoyote yale.... uwe mfano imara wa kuigwa

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni