Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Friday, August 15, 2014


Baada ya kupumzika kwa takribani miezi mitatu Ligi kuu ya Soka nchini England leo inaanza tena ukiwa ni msimu mpya wa mwaka 2014/2014.

 Kama ilivyokua msimu uliopita ambapo Manchester United walianza msimu kwa kucheza na Swansea vivyo hivyo msimu huu Man United wakiwa chini ya kocha mpya Luis Van Gaal watakua nyumbani Old Trafford kuikaribisha timu hiyo inayotoka katika visiwa vya Wales.
Hii ni mara ya kwanza kwa Kocha Luis Van Gaal katika heka heka za Ligi kuu England kwani hajawahi kufundisha wala kucheza.

Timu iliyopanda Daraja msimu huu Leicester City itakabiliana na Everton ambao msimu ulioisha walikua moto wa kuotea mbali.

QPR wakiwa wamerudi katika Ligi kuu msimu huu baada ya kushuka mwaka juzi watakua wenyeji wa Hull City.
Stoke City watakua nyumbani kuwakaribisha Aston Villa.

Katika jiji la London kutakua na mechi ya watani wa jadi kutoka jiji hilo ambapo Wagonga nyundo wa West Ham watakua Upton Park kuwakaribisha Totenham Hotspurs ambayo imepata kocha mpya.

West Brom wataialika Sunderland ambayo ilimaliza msimu uliopita kwa matokeo ya kushangaza wengi.

Mechi ya Usiku leo itakua mabingwa wa kombe la FA na Ngao ya Hisani Arsenal ambao wataialika Crystal Palace ambayo kocha wake Tony Pullis ameachia Ngazi kuifundisha timu hiyo.

RATIBA KAMILI LEO


  • Man United vs Swansea: 14:45
  • QPR vs Hull City: 17:00
  • Stoke City vs Aston Villa: 17:00
  • West Ham vs Totenham : 17:00
  • West Brom vs Sunderland: 17:00
  • Arsenal vs Crystal Palace : 20:30

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni