Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Friday, August 15, 2014

Wema Sepetu: Najuta Kumrudia Diamond



Takribani wiki sasa kumekuwa na taarifa zinazoeleza kuwa Miss
Tanzania 2006, Wema Sepetu hayuko sawa katika mahusiano yake ya
kimapenzi na nguli wa Bongo Fleva, Diamond Plutnumz….
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu na Wema, imefika mahali Wema anajuta
kuwa na Diamond kwa sababu ya kuandikwa kwa mambo mengi
yasiyo na ukweli na yanayomfedhehesha moyoni….
Rafiki huyo amedai kuwa mara kwa mara Wema amekuwa akijiuliza
sababu ya kuandikwa taarifa mbalimbali zisizo na kichwa wala miguu
ambapo mwisho wa yote hupata jibu ni kwa sababu ya kuwa na
mahusiano na Diamond….
“Wakati mwingine anasema angelijua bora angebaki bachela kwani kuna
kikundi cha watu hakipendi kumuona akiwa na Diamond hivyo
kinafanya kazi ya kumzushia taarifa zisizoeleweka kila mara kwa lengo
la kumshushia hadhi,” kimesema chanzo hicho
Mwandishi alipokiuliza chanzo hicho ni kwa kiasi gani Wema
“Ukweli ni kwamba Wema anampenda sana Diamond lakini hamwamini
kwa sababu wakati mwingine taarifa zinazoandikwa magazeti hutolewa
na Diamond mwenyewe, hali hiyo inampa wakati mgumu sana Wema
kujua ashike wapi na wapi apaache,”
“Unajua Diamond haaminiki, unaweza kukuta Wema anagombana na
watu kumbe mtoa taarifa ni Diamond mwenyewe.”

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni