Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Saturday, August 16, 2014

Hii ni kwa waqliohitimu vyuo tu



Salome alihitimu chuo kikuu na kuhangaika zaidi ya mwaka bila kupata kazi hata ile ya kujishikilia huku akiendelea kutafuta.

Maisha yakazidi kuwa magumu kwani hata nduguze kijijini nao waliamini kuwa kwa kuwa yupo mjini basi alikuwa na kipato cha kutosha.

Ile hali ilimpa wakati mgumu na kunakipindi akafikia kukata tamaa na kutaka kurudi kijijini ili akasaidiane na wazazi katika shughuli za shamba.

Akiwa kakata tamaa kabisa rafiki yake mmoja akampigia simu kuwa ofisini kwao anatafutwa binti wa mapokezi ( Receptionist) hivyo akapeleka cv yake huko na kisha akaitwa kwa ajili ya usaili.

Baada ya usaili akaambiwa atapigiwa simu kutaarifiwa kama amepata au la. Siku mbili baadae akapigiwa simu kuwa jumatatu yake aende kuanza kazi.

Alimshukuru Mungu na jumatatu yake akajiandaa na kuanza kwenda kazini kabla ya kupigiwa simu kuwa ile nafasi yake haipo tena kwani imefutwa kwa muda.

Salome alilia sana na kuona kama ni jaribu na aliporudi nyumbani akachukua biblia yake na kusoma Isaya 59:1 “Tazama mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia”

Akamshukuru Mungu hata kwa ile nafasi ya kuitwa tu na kuona kama ni baraka kisha akajilaza kwenye kochi lake apumzike.

Masaa mawili baadae akiwa katika usingizi mzito alishtushwa na mlio wa simu na namba ilikuwa ngeni.

Baada ya kupokea akaambiwa ni shirika moja la utafiti aliwahi kuomba kazi na sasa wana nafasi ya mtafiti kwenda mikoa 12 kufanya utafiti na itachukua mwaka mmoja na nusu na atalipwa 120,000 kwa siku kwa miezi mitatu ya kwanza ya filed na kisha ataajiriwa rasmi.

Salome alianguka chini kwa furaha na kusema maneno haya, "Tazama mwana nilikuita na sikio lako likasikia na ukanigusa kwa mkono wako wa baraka lihimidiwe jina lako takatifu..AMEN"

Rafiki, Mungu wetu anasikia pale tumuitapo. Mkono wa Bwana ukikugusa kamwe hutapungukiwa na kitu. Muelezo shida zako, furaha yako naye atakuwa pamoja nawe kwa kila kitu.

Sala yangu kwako

"Bwana Mungu nakuja kwako kwa unyenyekevu kabisa nikiomba mkono wako wa baraka usinipungukie.

Wewe utendaye miujiza kwa wengi, naomba usinipite Bwana kwa maana nakuhitaji sana.

Sikiliza kilio cha moyo wangu Bwana na ukanibariki sawa sawa na mapenzi yako.Amen"

Commment AMEN na share kuifanya sala hii itende miujiza katika maisha yako

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni