Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Saturday, August 16, 2014



Sura hiyo hapo ni ya mwanaume. Bila shaka umeshawahi kukutana na sura kama hii katika maisha yako. Kama hujawahi kukutana nayo huenda kuna siku utakutana nayo. 


Mwanaume mwenye sura kama hii ana tabia zifuatazo:

Ni wanaume wasiopenda tabu tabu wala vurugu. Kwa hiyo wanapenda utulivu na maisha ambayo yana nafuu kwao. Ni watu wenye mvuto katika kupenda na kupendwa. Hii ina maana kwamba, mwanaume mwenye sura kama hiyo hapo juu asipokuwa mwangalifu anaweza kujikuta akiwa ana lundo la wapenzi kwa sababu wanawake wengi hupenda kushobokea wanaume wenye sura kama hiyo.

Ni watu wenye kufikiria haraka au kutathmini kujua zile faida wanazoweza kuzipata kupitia kwa mtu ambaye wako naye, awe mpenzi au rafiki. Hii ina maana kwamba, wanaume wenye sura kama hiyo wana urafiki wa mradi.

Wanaume wenye sura kama hiyo hupenda mazungumzo yanayohusu utajiri, na huo ndio mtaji unaowafanya wanawake wawashobokee kwa sababu wanawake wengi hupenda kujihakikishia usalama wa kulindwa na kwa sababu usalama siku hizi maana yake ni kuwa na fedha hivyo kwa kusikia mazungumzo yao yanayohusu utajiri wanajua wamelamba dume.

Lakini pia ni kawaida ya wanaume wenye sura kama hiyo kutafuta utajiri zaidi kuliko kitu kingine. Kama unataka kuwa na urafiki na mwanaume mwenye sura kama hiyo basi inabidi katika mazungumzo yenu uzungumzie utajiri na mbinu za kuupata.

Ni watu wenye kutawaliwa na tamaa ya kumiliki vitu vya anasa au vya starehe. Wanapenda kuwa na samani za ndani za gharama kubwa na hata gari, tena gari lenyewe liwe la gharama na la kipekee. Huwa wanajua mambo mengi sana mazuri , yaani vitu vizuri vya burudani na starehe. Ni watu wa kujirusha na wanatokea kuyajua maeneo ya kujirusha ya matawi ya juu.

Ni watu ambao katika kupenda, huwapenda wanawake wenye maumbile makubwa, hasa makalio. Lakini hata hivyo wana kasoro ya kuacha sana katika uhusiano, yaani hawadumu sana na wapenzi. Kama mwanaume mwenye sura hiyo akidumu na mpenzi, basi vurugu na tafrani vitatawala ndoa au uhusiano wake.

Ni watu ambao wana bahati au uwezo wa kipato kikubwa kwa sababu ni wachakarikaji wazuri wa kutafuta ngawira, lakini wengi wao hushindwa kutunza kipato chao kwa sababu wanapenda anasa na kujirusha na wanawake hasa wenye makalio makubwa.

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni