Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Sunday, August 17, 2014


Gari la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), lililokuwa likisafirisha maiti 10 za watu kwenda katika
Hospitali ya Mtakatifu Francis Ifakara, wilayani Kilombero, limewagonga watu wawili waliofariki
dunia papohapo, eneo la Mtego wa Simba, Mikese mkoani Morogoro.
Waliokufa katika ajali hiyo iliyotokea saa 5:25 asubuhi jana ni dereva na abiria wa bodaboda.
Maiti hizo zilizokuwa zimehifadhiwa katika mifuko maalumu ya plastiki, zinaelezwa kuwa zilikuwa
zikipelekwa katika Hospitali ya Mtakatifu Francis, ili zitumike kwa mafunzo.
Akizungumzia ajali hiyo katika eneo la tukio, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa
Morogoro, Boniface Mbao alisema kuwa gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Pankrasi Pascal, mkazi
wa Ifakara, wilayani Kilombero.
Mbao aliwataja waliokufa kuwa ni Shaaban Rajabu na Ally Benulo, wakazi wa Kijiji cha Mikese,
waliokuwa wamepakizana kwenye pikipiki.
Tukio hilo limekuja siku kadhaa baada ya mabaki ya miili ya binadamu kugunduliwa ikiwa imetupwa
katika dampo moja lililoko Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni