Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Sunday, August 17, 2014


Alikiba anataka watu wafahamu kuwa hana na tatizo na Diamond Platnumz na
amewataka watu waache kuwakosanisha.
Akizungumza na Bongo5 leo, AliKiba amewataka watu kuachana na tabia ya
kuwagombanisha Diamond ili wafanye muziki mzuri.
“Kila mtu anaandika anachotaka juu ya mimi na Diamond, mpaka wengine
wanatumia akaunti fake za Facebook kutukosanisha, ndio maana nikasema
kuna wengine wanafanya for fun na wengine wanafanya ili kutukosanisha
wengine wanafanya lakini hawajui wanachofanya,” amesema Alikiba.

“Mimi najaribu kuwaomba wadau mbalimbali waache hiyo tabia ya
kutukosanisha kwa sababu mimi sina ugomvi na Diamond na wala sina
mambo hayo. Ninachowataka waendelee kusupport kazi zetu ili mambo
yaende vizuri kwa sababu sisi ndo wasanii wao tunaoiwakilisha Tanzania.
Wanapotupa moyo wao sisi tunazidi kukaza buti ili tufike mbali zaidi. Watu
wanaotengeneza ugomvi wangu na Diamond waache cha zaidi wafanye
kusupport muziki na watuambie ni mapungufu gani ambayo yamepungua ili
tujirekebishe,” ameongeza.
Katika hatua nyingine, Alikiba amezungumzia mapokezi ya wimbo Mwana na
Kimasomaso pamoja na ujio wa video zake.
“Kwanza watu wamenipokea vizuri sana kama nilivyokuwa nikitarajia,
imeonyesha ni jinsi gani yale malalamiko ya maana walikuwa wakilalamika
kwamba nimekumiss na nilivyotoa nyimbo watu wanasikiliza na kuinjoy na
nyimbo zenyewe zimekuja wakati mzuri na zenye maadili mazuri ya kuelimisha
na kuchezeka na ya kufurahisha. Maandalizi ya video yapo tayari na booking
ipo tayari vilevile, maandalizi nimeandaa hata kabla sijatoa nyimbo, video
itafanyika nje na moja ni hapa siwezi sema ni nchi gani bado ni mapema
nitasema baadae nikishaitoa, kwasababu nimetoa track mbili moja itafanyika
hapa na nyingine itafanyika nje.”

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni