Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Wednesday, August 27, 2014



Stori: Musa Mateja na Shakoor Jongo
MAKUBWA! Mambo yamekuwa mambo, kadi ya gari jipya la staa wa sinema
za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ imeibua mazito kufuatia Jeshi la
Polisi Dar es Salaam kubaini kuwa namba ya Sanduku La Posta (SLP)
iliyoandikwa kwenye kadi hiyo ni Wizara ya Mambo ya Ndani Tanzania.
IMEVUJAJE?!
Hilo lilibainika baada ya gazeti dada na hili, Ijumaa toleo la Ijumaa iliyopita
kuandika habari yenye kichwa kisemacho; LULU AANDIKA HISTORIA.
Katika habari hiyo, Lulu alipewa shavu kwa vile alinunua gari aina ya Toyota
Rav 4 New Model kwa pesa zake mwenyewe tofauti na baadhi ya mastaa wa
Bongo ambao huhongwa magari na wanaume.
SIMU YAPIGWA
Wakati gazeti hilo likiwa mitaani, mtu mmoja aliyedai kuwa ni afisa wa jeshi lapolisi jijini Dar es Salaam alipiga simu kwenye chumba cha habari cha Global
Publishers na kusema kuwa S.L.P ya 9140 iliyotumika kwenye kadi ya gari la
Lulu ni ya jeshi hilo

NI KOSA LA JINAI
Ofisa huyo aliliambia gazeti hili kuwa raia wa kawaida haruhusiwi kutumia
sanduku la barua la jeshi kitu alichodai kinaonesha jinai ilifanyika wakati wa
usajili ya gari hilo.
“Haiwezekani Lulu atumie Postal Office Box (P.O.Box au S.L.P) ya jeshi
kwenye kadi ya gari lake ikizingatiwa kuwa yeye ni raia wa kawaida.
“Ukiachana na hilo hata sisi maofisa wa jeshi la polisi hatuwezi kuitumia hiyo
anuani kwa shughuli zetu binafsi labda kuwe na kibali maalum,” alisema afisa
huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa vile yeye si msemaji wa jeshi
hilo.
LULU ANASEMAJE?
Baada ya kupata maelezo hayo, gazeti hili lilimtafuta Lulu ili kujibu madai hayo
yenye utata ambapo alisema kuna mtu alimtengenezea namba yake ya TIN
(Taxpayer Identification Number) ndiye aliyemwekea anuani hiyo bila yeye
kujua.
Huku akisita kumtaja kwa jina mtu huyo lakini akimtaja kwa cheo ambacho
kiko wazi na mapaparazi wetu wakamjua, Lulu alifunguka hivi:
“Namiliki gari langu kihalali kabisa na nina kila kitu, niko tayari kwenda kokote
kuonesha uhalali wa umiliki wangu. Kuhusu hiyo anuani, mtu
aliyenitengenezea TIN Number ili nipate leseni ya udereva ndiye aliyetumia
hiyo anuani, mimi sijui chochote jamani.”
AOMBA AHIFADHIWE SIRI
Katika hali ya kushangaza, Lulu aliwaambia mapaparazi wetu wasimtaje jina
gazetini mtu huyo aliyemsajilia TIN akisema asitiriwe siri yake
POLISI NAO WANENA
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, ambako ndiko usajili wa gari hili
ulifanyika katika ofisi za TRA, Zakaria Sebastian, alisema jeshi lake halina
taarifa za kuwepo kwa jambo hilo lakini watalifuatilia kwa karibu.
“Huenda ni mke wa askari au mwanafamilia. Unajua kuna baadhi ya maofisa
wana msamaha, huenda alitumia hivyo, lakini tutafuatilia,” alisema kamanda
huyo ambaye alielezwa kuwa, Lulu hajawahi kuwa mke wala mwanafamilia ya
mwajiriwa wa jeshi la polisi.
“Kama hajawahi kuwa mwenye kustahili kutumia anuani hii, basi tutafuatilia ili kujua wakati akiitumia, je alikuwa anakusudia kufanya jinai? Tukijiridhisha
hivyo bila shaka sheria itafuata mkondo wake.”
GPL

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni