Karrueche Tran amewaomba radhi mashabiki wa Beyonce waliomshambulia
kwenye mitandao ya kijamii baada ya kudiss muonekano wa nywele za Blue
Ivy kwenye tuzo za MTV VMAs, wakati akifanya kipindi cha 106& Park cha
BET.
Karrueche aliponda muonekano wa nywele za Blue Ivy katika kipengele cha
kipindi hicho kilichopewa jina la ‘Top 6 Things Blue Ivy thought about the
VMA’s’, ambapo alisikika akisema kwa kumkariri Blue Ivy kuwa ‘Kweli niliamka
hivi kwa sababu wazazi wangu hawakunichana nywele. Pole Blue!
Nakupenda!”
Mashambulizi yaliyoendelea ndani ya siku mbili mfululizo yamemfanya
mrembo huyo kuomba radhi kupitia Instagram akikiri kufanya makosa kwa
kuwa yeye ni binadamu.
Katika maelezo yake, ameomba radhi kwa kutamka sentensi hiyo ambayo
amesema ilitengenezwa kwenye muongozo wa kipindi na BET na ikapitia
kwake.
BET wamewajibika pia na kueleza kuwa Karrueche alikuwa anasoma
maelezo hayo kwenye teleprompter (screen ya kusomea habari kwenye TV)
kama sehemu ya script na kwamba ilifanyiwa mabadiliko dakika kumi kabla ya
kwenda hewani na hakupata nafasi ya kuipitia tena.
Huenda angekataa kuisoma kama angeipitia awali
0 comments:
Post a Comment