Staa wa kike wa filamu bongo, Aunt ezekiel,
ambaye ni shoga mkubwa wa miss tanzania
2006 wema sepetu ameibuka na kutamka
bayana yeye si mpambe wa mrembo huyo,
wala sio mbeba mikoba wake na wala haishi
kwa kusubiri pesa zake anazohongwa na
Diamond.
Staa huyo alifunguka kuwa yeye hausiki na
kumpeleka mwenzake kwenye starehe
kwani wote huenda kwa matamanio yao
binafsi, Aunt aliwaponda wote waliokuwa
wakimuhusisha na kauli ambayo ilitolewa na
Diamond kwamba wema anapotezwa na
mashoga zake wapenda starehe.
" wajinga wakubwa, watu wananihusisha
mimi na masuala ya wema na Diamond.
Mimi ni staa mkubwa na wema ni staa ,
nimeanza kuhangaika na maisha mda mrefu
sio mpambe wa wema , kwanza ana nini
cha ziada cha kunipa hadi niwe mpambe
wake?
Nina maisha yangu na miradi yangu toka
kitambo, kama kwenda kwenye starehe
wema anaenda kwa matamanio yake na
mimi na matamanio yangu, siishi kwa
sababu ya pesa za diamond wala wema,
masuala yao ya mapenzi hayanihusu kabisa,
wayaongee wayamalize kama kuchukua
hatua wachukue sio kuongelea pembeni,
mimi sibembelezi urafiki kwa sababu
ninayamudu maisha na ni STAA.
Tena ole wao wanaonijua aunt na
mihangaiko yangu siwezi kufikiria ujinga
huo, sitegemei hela ya wema wala diamond
wake, wakome kabisa tena wanikome na
iwe mwisho" Alisema staa huyo aliyefanya
vizuri kwenye movie ya Young billionaire.
Saturday, August 23, 2014
Aunty ezekiel: Wema Hana Msaada Wowote kwangu na Wala Mimi Sio Mbeba Mikoba Yake
Posted by Unknown on 3:12 PM with No comments
Categories:
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment