Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Saturday, August 23, 2014

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),
imetoa onyo pamoja na kutoza faini ya
takribani Sh milioni 5 kwa kituo cha redio na
televisheni cha Clouds, kwa kukiuka kanuni
za utangazaji za mwaka 2005.
Wakielezea uamuzi huo jana jijini Dar es
Salaam, Kamati ya Maudhui ya mamlaka
hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake,
Margaret Munyagi ilisema kuwa ukiukwaji
wa kanuni hizo ulifanywa kwa nyakati
tofauti na vituo hivyo.
Alisema kwa upande wa kituo cha redio cha
Clouds, kupitia kipindi chake cha ‘Njia
Panda’ kilichorushwa hewani Juni 15 mwaka
huu kati ya saa 8.00 mchana na saa 10.00
jioni kilikuwa na mada iliyohusu safari ya
kuzimu ambapo maudhui yake yalijaa
simulizi za kufikirika, za kishirikina na
kichawi.
Aidha alisema kosa lingine kituo hicho
hakikufuata kanuni za Utangazaji(maudhui)
za mwaka 2005 zinazowataka kuwasilisha
ratiba ya vipindi vyao kwa TCRA ili
viidhinishwe na vilevile kuvichapisha katika
gazeti kabla ya kurushwa hewani ambapo
kipindi cha Njia Panda hakikuwasilishwa kwa
ajili ya kuidhinishwa.
Wakati huo huo, kituo cha televisheni cha
Clouds kilirusha kipindi cha ‘Bibi Bomba’ Mei
16 na Juni 6 mwaka huu kati ya saa 3.00 na
saa 4.00 usiku ambacho kilikiuka kanuni za
Utangazaji (maudhui) za mwaka 2005.
Alisema kipindi hicho kilidhalilisha mabibi
hao walioshiriki pamoja na wanawake kwa
ujumla kutokana na maswali ya aibu
waliyokuwa wakiulizwa na waamuzi wa
shindano hilo ambayo ni kinyume na kanuni
hizo.
Aidha alisema kituo hicho kinatozwa faini ya
Sh milioni moja na kutakiwa kuwasilisha
TCRA mwongozo wa kuchuja na kusimamia
maudhui yasiyofaa kabla ya kutangazwa.
TCRA imesema kama Kanuni za Utangazaji
zitaendelea kukiukwa hatua kali zaidi za
kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni