Ulichokuwa ukisubiri kwa muda mrefu huenda
kikatokea hivi karibuni. Collabo ya Alikiba na
Diamond Platnumz mabibi na mabwana inanukia.
Akizungumza na kipindi cha Jahazi cha Clouds FM
leo (20/8), Alikiba amesema upo uwezekano wa
kufanya kazi ya pamoja kama kukitokea mabadiliko.
“Mawazo ya kolabo yapo, mawazo unapata mengi
tu, hiyo nimeshaisikia vilevile, na wewe sio mtu wa
kwanza kuniuliza hicho kitu kipo. Lakini muziki vile
vile kama unavyoona kuna mavazi na style, vazi hili
linatakiwa liende disko hili ni vazi la beach, vazi hili
la ofisini, vazi hili la mpirani, hili la mchangani, hili
la kwenye ukumbi unajua vitu kama hivyo! Kwahiyo
Diamond akipata vazi lake ambalo linahusiana na
vazi ambalo natakiwa nivae, hakuna tatizo
tunafanya kazi kama kawaida, kwa sababu yeye
anafanya kazi vizuri,” alisema AliKiba.
Alipoulizwa kama kuna uwezekano wa kufanya show
kubwa na Diamond alijibu kwa kicheko: “Wewe hujui
kama watu wanasubiria (show) au unajisahaulisha.”



0 comments:
Post a Comment