Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Tuesday, August 19, 2014

AISHA BUI: KUSHINDA MAISHA UWE MKAKAMAVU

Stori: Mwandishi Wetu
MWIGIZAJI wa filamu anayekuja juu nchini, Aisha Bui, amesema ili kuyashinda maisha magumu Bongo, ni lazima uwe mkakamavu, kama yeye alivyolazimika kwenda kutengeneza filamu yake mpya ya Mshale wa Kifo, katika msitu wa kutisha ili kwenda tofauti na wengine.
Mwigizaji wa filamu anayekuja juu nchini, Aisha Bui.
“Nilijitoa maisha yangu kwa kuingia msituni kutengeneza filamu ya mapigano porini, kutafuta uhalisia, najua nina deni kwa wapenzi wa kazi zangu, wanajua kuwa mimi ni bora hivyo lazima niwe bora kila mwaka,”anasema mwigizaji huyo.
Alisema maoni mengi ya watu yanaonyesha wanakerwa na kila filamu kuigizwa mijini tu, hivyo yeye akajitoa ili aende sambamba na mahitaji ya mashabiki wake, kwa kwenda katika misitu ya Morogoro vijijini kuifanya filamu hiyo, aliyowashirikisha pia Mzee Chilo, Salim Ahmed ‘Gabo Zagamba’ na wengineo, kazi iliyofanywa  Yuneda Entertainment.

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni