Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Monday, August 25, 2014


Tumepanda daladala moja, ikafika wakat wa konda kuchukua mchango wa
mafuta....kimbembe kikaanzia hapo, mdafada kajisachi weeeee nauli hana
akaanza kumbembeleza konda kuwa atamlipa akifika mwisho wa safari.

Konda akagoma na akaanza kutoa maneno ya dharau kwa yule dada,
nikaona hapa ndo nakamatia fursa, nikamlipia yule demu halafu nikamchimba
mkwara mzito sana konda huku nikitishia kumtandika na makofi, nikajifanya
namfahamu sana yule dada.

Lengo langu ni kwamba tukishuka nachukua contact fasta, maana kwa kweli
demu alikuwa ni mkali kinoma, tulipofika mwisho wa safar akaniomba
tuongozane, nikajua yees kumbe hata yeye kanimaindi....tukafika kwny duka
flani.

Nikasikia analiambia jamaa flan tuliolikuta pale dukani:- baby yani nilitaka
kuadhirika....asingekuwa huyu hata cjui ingekuwaje, akalisimulia kila kitu huku
kajiegesha kwny kifua cha huyo boya, mi natukutia kwa hasira, alipomaliza
kulisimulia likambusu mdomoni.

Halafu eti likanipa mkono kunishukuru, likatoa wallet na kunipa sh elfu tano,
ina maana huyo dada alidhani nimemkopesha ile mia nne,au alitaka
kunidhalilisha mbele ya yule boya.

Ina maana yeye hawezi kujiongeza kuwa kuna mengineyo nilitaka yaendelee
behind the scene, au alijua mi ni mlokole, au alitaka nijue ana mtu wake,
mxxxxxxxxxiiiiiiiuuuu, bado nina maswali mengi sana juu ya hilo.



0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni