Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Monday, August 25, 2014


Wanasaikolojia wakiongozwa na mwanasaikolojia Benedict Jones
wamegundua kwamba, mwanamke akitaka kupima uzuri wa mwanaume
ambaye angependa kuwa rafiki au mpenzi wake, hupenda kujua kama hata
wanawake wenzie wanampenda kama yeye anavyompenda……..

Anavyozidi kuwaona wanawake wenzie wakitabasamu au kumchekea
mwanaume huyo anapopita mbele yao ndivyo atakavyojua kwamba, huyo
mwanaume ni mzuri.

Hali hii inafahamika kama copycat reflex na ni matokeo ya nadharia ya Darwin
ya mambo ya mabadiliko ya maumbile ya viumbe, kwa mujibu wa wataalamu
hao, yaweza kutumika pale ambapo mwanamke anakumbana na wanaume
wengi wanaomtaka lakini anapata matatizo ya kumchagua yupi na kumwacha
yupi.

Au akiona uchaguzi wa mwanaume bora utamchukulia muda wake mwingi na
nguvu zake hujirahisishia kwa kuchukua uamuzi wa kuwaangalia wanawake
wenzie wanavyomwona mchumba wake mtarajiwa.

Uchunguzi huu hufanyika bila wanawake wenzie kujua kwa hiyo mwanaume
anayeonekana kuchangamkiwa sana na wanawake wenzake kwa lengo la
kumvuta ili awe mpenzi wake ndiye ambaye atapata uwezekano mkubwa wa
kukubaliwa na mwanamke huyo.

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni