Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Friday, September 19, 2014

KAJALA Akwama PESA ya Kumtoa Mumewe Jela

Licha ya mkwanja kumtembelea, msanii wa
filamu Bongo, Kajala Masanja amekwama
kupata pesa ya kumlipia faini mumewe Faraji
Chambo ili aweze kutoka jela.
Akizungumzia ombi la mumewe huyo
kumtaka kutofuja pesa badala yake amlipie
faini ili aondokane na mateso ya gerezani,
Kajala alisema ni kweli anampenda sana
mumewe na angetamani kufanya hivyo lakini
kiasi cha shilingi milioni 200 kinachotakiwa si
kidogo hivyo hawezi kukipata.
“Nampenda sana mume wangu, hilo halina
ubishi na pia najua anateseka sana kule
gerezani kwani nakujua lakini milioni 200 siyo
hela ndogo ujue. “Natamani hata leo niwe
nayo nimlipie lakini ndiyo hivyo tena,”
alisema Kajala kwa masikitiko.
Hata hivyo, licha ya Kajala kuwa na nia ya
kumtoa jela mumewe, mmoja wa mawakili
aliyekuwa akihusika na kesi yao aliyeomba
hifadhi ya jina lake alisema:
“Kama Kajala anafikiria kumlipia mumewe
faini simshauri afanye hivyo kwani hukumu
iliyotolewa ni ya kesi moja na ile nyingine ya
kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa bondi na
Takukuru, bado inaendelea na huwa Faraji
anatoka gerezani kwenda mahakamani.
“Sasa Kajala anaweza kutoa pesa zake,
mumewe akatoka lakini hukumu ya ile kesi
nyingine ikatolewa na akarudi tena jela,”
alisema wakili huyo. Hivi karibuni, mume wa
Kajala alituma ujumbe kupitia watu
wanaokwenda kumtembelea akimtaka mkewe
kumuonea huruma na kumlipia faini ili atoke
gerezani badala ya kuzitumia pesa kwa
anasa.

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni