Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Saturday, September 20, 2014

Barua fupi kwa Bill Gates

Kwa: Bill Gates, Microsoft

Kutoka kwa: Antonia Milinga, Tanzania
Tarehe: 4 October 2013

Yahusu: Matatizo kwenye kompyuta yetu mpya.

Ndugu Bill Gates, Anko wangu amenunua kompyuta mpya kwa ajili ya kutumia nyumbani kwetu.

Nilipoichunguza nimegundua ina matatizo kadhaa. Nimeamua kukuandikia barua hii ili uyafanyie kazi.

1. Kuna batani ya 'start' lakini hakuna batani ya 'stop' button. Tafadhali tazama kwa makini.
2. Nina mashaka kama umeweka 're-guta' maana nimeona umeweka tu 're-cycle', lakini nyumbani kwetu kuna guta na siyo baskeli.
3. Pia nimeona kuna sehemu ya 'Find' lakini wala haifanyi kazi. Anti yangu jana alipoteza funguo. Nimejaribu sana kubonyeza find ili itusaidie kutafuta funguo imeshindwa. Naripoti tatizo hili.
4. Nimeona tu kuna 'Microsoft word' sasa nataka kujifunza 'Microsoft sentence', sasa ni lini utatuwekea Microsoft Sentence?
5. Tumenunua CPU, mouse na keyboard, lakini kuna kipicha kimoja tu kinachoonyesha 'My Computer': lini utatuwekea vipicha kwa ajili ya hivyo vifaa vingine?
6. Nimeshangaa kuona kompyuta imeandika mahali 'MY Pictures' lakini sijaona picha yangu hata moja humo. Lini mtaziweka?
7. Pia mmeweka 'MICROSOFT OFFICE' inakuwaje kuhusu 'MICROSOFT HOME' kwa kuwa hii ni kompyuta tunayotumia nyumbani kwetu na wala siyo ofisini.
8. Pia umeweka 'My Recent Documents'. Vipi kuhusu 'My Past Documents'?
9. Pia umeweka 'My Network Places'. Tafadhali sana iondoe hiyo maana anko atakuwa anajua mahali nilipo, kuna siku huwa natoroka shule.

Jambo la mwisho. Wewe jina lako ni GATES sasa kwa nini umeamua kuuza WINDOWS?

Wasalaam,
Antonia.

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni