MKALI wa ngoma ya Johnny, Yemi Alade, hataweza kutua Bongo leo kama ilivyotarajiwa na badala yake ataingia nchini kesho Jumatano, Agosti 6, 2014 saa tano usiku tayari kwa kukinukisha kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini ambalo limebakiza siku chache kabla ya kutimua vumbi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Agosti 8, 2014.
Akiongea na mtandao huu, mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto alisema Alade anatarajiwa kutua kesho kwa ndege ya Shirika la Kenya Airways akitokea Lagos, Nigeria na kuwataka mashabiki wa mwanamuziki huyo, kujitokeza kwa wingi kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.
0 comments:
Post a Comment