Stori: Makongoro Oging’
KWA mara nyingine tena makachero wa polisi wamefanikiwa kumnasa trafiki feki ambaye anadaiwa kutikisa Jiji la Dar es Salaam kwa ukamataji wa magari na kuwatoa fedha madereva, Uwazi lina mchapo kamili.
Chanzo chetu ndani ya jeshi la polisi, kinaeleza kwamba trafiki huyo feki anayejulikana kwa jina la Robinson Seif (30) anayejifanya kuwa na cheo cha staf sajenti alikamatwa juzi Jumamosi akiwa ‘kazini kwake’.
Chamazi - Temeke jijini Dar es Salaam baada ya kupatikana kwa taarifa zake.Chanzo hicho kilidai kwamba askari huyo aliwahi kuwa polisi wa usalama barabarani Kibaha mkoani Pwani lakini alifukuzwa kwa kukosa sifa ya kuendelea na kazi hiyo.
Inadaiwa kuwa, baada ya kuonekana na makosa mbalimbali jeshi la polisi lilimfikisha katika mahakama yao na akapewa adhabu ya kuachishwa kazi.“Madereva wameshangilia sana, ni kama sherehe tu kwao, maana jamaa amewapiga mabao sana akijifanya ni trafiki,” kilipasha chanzo hicho.
Sura ya ‘karibu’ ya askari huyo feki aliyekamatwa, Robson Seif Mwakyusa.
Sura ya ‘karibu’ ya askari huyo feki aliyekamatwa, Robson Seif Mwakyusa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, ACP Kihenya Kihenya amekiri kukamatwa kwa askari huyo na kwamba alikutwa yupo katika kazi zake hizo akijidai kuwa askari wa usalama barabarani.
“Huyu Seif amekuwa akiwadanganya wananchi kuwa yeye ni trafiki na kuwachukulia fedha, sare alizokutwa amevaa ni zetu lakini bado tunachunguza alipozitoa, pia tunafuatilia mambo mengine, nitatoa taarifa kamili baadaye,” alisema Kamanda Kihenya.
Kova akionyesha baadhi ya sare za jeshi la polisi alizokamatwa nazo polisi huyo feki.
Kova akionyesha baadhi ya sare za jeshi la polisi alizokamatwa nazo polisi huyo feki.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Ulrich Matei, alipoulizwa kwa njia ya simu alikiri Seif kuwahi kufanya kazi mkoani Pwani huku akifafanua kuwa ni kati ya askari nane waliofukuzwa kazi Januari mwaka huu kwa makosa mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment