Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Sunday, August 24, 2014

wewe usiniambie mama mwajuma anafanya kazi hapa

Jamaa mmoja kipofu kaenda mgahawani, alipofika akaletewa orodha ya misosi ila akamwambia meneje: mimi ni kipofu, siwezi kuona. 

Nenda jikoni niletee kijiko ambacho kimetumiwa lakini hakijaoshwa. Nitakinusa halafu ntakwambia nataka chakula gani. Meneja akashangaa ila akaenda akamletea, kipofu akakinusa akamwambia meneja: nataka hiki kinachonukia, viazi na nyama. Hivyo hivyo. Meneja akashangaa kwamba kweli mteja aliyetumia kile kijiko alikula viazi na nyama. Basi jamaa akaletewa msosi akala akaondoka zake. 

Siku ya pili akaja mchezo ukawa ule ule, ananusa kijiko, anapatia analetewa msosi, anakula anasepa. Siku ya tatu meneja wa hoteli akamwambia mkewe ambaye alikuwa ndo mpishi: yule kipofu akiji leo ngoja nimjaribu. Mchana ukafika kipofu akaenda kuagiza msosi. Meneja akaenda jikoni akamwabia mkewe (alikuwa anaitwa Mwajuma) hebu weka hiki kijiko kwenye kwapa lako, ni kisafi, kiwe tu na harufu yako. Wife akakubali, akakiweka kwapani, kipofu akapelekewa. Kipofu akakinusa halafu akasema: Sikujua kama Mwajuma anafanya kazi hapa!

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni