Rapper wa kike na member wa zamani wa Terror Squad amewataja baadhi ya wasanii waliompa msaada na kuwa pamoja nae alipokuwa jela.
Katika mahojiano aliyofanya na BET, rapper huyo amemtaja 50 Cent kuwa sehemu kubwa ya msaada wake hasa pale alipokuwa anataka kukata rufaa ya maisha ya jela. Amesema kiongozi huyo wa G-Unit alisaini barua zake zaidi ya mara moja kwa kuwa alikuwa anaamini atakapotoka jela atapata kazi na hiyo itakuwa njia nzuri ya yeye kukaa mbali na matatizo.
Amewataja pia Keyshia Cole, French Montana, Rick Ross na Jadakiss kuwa wasanii ambao alikuwa akiwasiliana nao sana katika kipindi chote alipokuwa jela akitumikia kifungo cha miaka 6.
“Nadhani waliguswa na hali yangu. Hawakuwa wananiangalia kama Remy Ma rapper. Nilikuwa Remy na chochote unachotaka nakuelewa. Na nilikuwa sihisi kama mtu yeyote niliyekuwa naongea nae alikuwa fake au walikuwa wanasema vile kwa kuwa nilikuwa naongea nao kwenye simu.” Amesema Remmy Ma.
Remy pia amegusia kuhusu beef kati ya Lil Kim na Nicki Minaj na kuwashauri rappers hao kutafuta jinsi ya kuyamaliza kwa kuwa anaamini wanauwezo wa kufanya hivyo.
“Kutokana na kile nilichokiona, beef iliyotokea kati ya Lil Kim na Nicki Minaj , nadhani ni kitu ambacho wao wanaweza kukimaliza. Sidhani kama nitakuwa na uwezo wa kuingilia.” Ameongeza.
“Ni kama mimi, kila nachosema kwenye record, natakiwa kuwa naongea kuhusu Nicki Minaji. Ndivyo kila mtu anavyosema. Lakini hauongei kuhusu mtu yeyote. Unatakiwa kusema wewe ndiye mkali zaidi. Unatakiwa kusema wewe ndio Malkia wa rap.” Ameeleza Remy Ma.
Wakati akiwa jela miezi michache kabla hajaachiwa rasmi, Remy Ma alifanya mahojiano na Billboard na kueleza kuwa tayari wamemaliza beef kati yake na Fat Joe, walimaliza kila kitu kwa njia ya simu.
“I just recently spoke to him and we had a wonderful conversation. It started off a little awkward. We're both like, 'Just say what you want to say.' We were both holding on to our egos. 'Well what do you want to say?' 'No what do you want to say?' We finally let it go. We ended up talking about things I want to do when I get home. He said, 'I still think you're the dopest female rapper ever.' I'm like, 'Really?!' When you put egos and pride aside, and be the real people that you are it works out… I told him that when I do go home I'm going to make it my business that we talk more.”
0 comments:
Post a Comment