
Msanii underground mkongwe Nyandison Morali anatarajia kuachia track moja matata sana ienfayo kwa jina la Mboga za Majani aliyomshiriksha msaani chipukizi Mtafya wa jijni Mbeya.

Akiongea na Uvunguni Mwetu Blog Nyandison alisema, " Hii ni track ambayo inalengo la kuwahamasisha vijana kupenda afya kwakula mboga za majani hasa katika nyakati hizi ambazo vijana wengi wanakuwa busy na maisha na kula vyakula visivyokidhi haja ya miili yao kiafya, na nadhani hii itakuwa ni ngoma nzuri ambayo nimeifanya mwaka huu"
Kwa upande wa ushiriki wa Mtafya katika ngoma hii, Nyandison alisisitiza kuwa wakazi wa mbeya wajiandae kupata ladha nzuri kutoka kwa mkali wa kibao cha kutukuyu kusouth.
Kwa habari zaidi tembelea Morali Hodari


0 comments:
Post a Comment