Kwa mara ya kwanza staa wa Bongo Fleva, Emanuel Elibariki ‘Nay wa
Mitego’ ameibuka na kuuelezea upande wa pili wa maisha yake kuwa kabla
hajawa mwanamuziki alikuwa mwizi balaa!
Akizungumza na mwandishi wetu ana kwa ana jijini Dar es Salaam juzi, staa
huyo alikiri kupitia katika majanga kibao maishani mwake likiwemo la kulala
katika vituo mbalimbali vya polisi vya jijini Dar kufuatia kufanya matukio ya
uhalifu.
“Kwanza kabisa nilikuwa nalala Feri na watoto machokoraa. Nilikuwa naona
ndiyo maisha japokuwa nilijua kuna maisha mengine mazuri zaidi lakini
ningeyapate?
“Dah! Yaani kusema kweli nilipita kwenye majanga makubwa sana jamani!
Anyway, kimsingi ukweli wa maisha yangu siwezi kuuficha maana nitakuwa najiongopea bure kwani ni kweli niliishi katika maisha ya matukio sana,”
alisema Nay.
Akizidi kutiririka , Nay ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wa Mr Nay
aliweka bayana kwamba kwa nyakati tofauti aliwahi kuiba vitu mbalimbali
(hakupenda kuvitaja) kwa watu wa karibu yake akiwemo Prodyuza Paul
Mathysse ‘P Funk’ na kwenye studio moja iliyopo maeneo ya Mwenge jijini
Dar.
“Enzi zangu nilikuwa balaa, Majani mwenyewe (P. Funk) nilishawahi kumliza,
nakumbuka pia kuna jamaa zangu walikuwa na studio ya muziki pale Mwenge
nao niliwapiga.
“Tena hawa jamaa wa studio nakumbuka walikuja kinitaiti nikiwa kwenye
msiba, wakanitia pingu na kunipeleka kituo cha polisi lakini bahati nzuri
marehemu John Mjema, alikuwa mshikaji wangu sana, akaja kunitoa,”
alisema Nay.
John Mjema ‘Bomba la Mvua’ alikuwa mwanamuziki wa Kizazi Kipya, alifariki
dunia Februari 10, 2008 kwa kujichoma kisu cha shingo nyumbani kwake
Mtoni Kijichi jijini Dar.
Nay akaongeza: “Kulala polisi nadhani ni kama mara saba hivi na mara zote
aliyekuwa akinitoa ni John Mjema. Yeye wakati ule alikuwa akifanya kazi kule
maeneo ya Feri.”
Pamoja na matukio hayo ambayo Nay ameyafanya, alisema alishatubu na
kumwomba Mungu amsamehe kwani anaamini ujana ndiyo ulikuwa
ukimsumbua.
“Yaliyopita si ndwele, kwa sasa naganga yajayo maana muziki unanilipa na
naendelea na harakati zangu kama kawaida, nilishasahau hayo matukio ya
ajabuajabu,” alimaliza Nay.
Miongoni mwa mafanikio makubwa aliyoyapata msanii huyo kupitia muziki wa
Bongo Fleva ni kujenga nyumba Kimara-Rombo jijini Dar na gari la
kutembelea aina ya Nissan Murano
0 comments:
Post a Comment