Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Saturday, August 9, 2014

Kweli dunia ina mambo! Kuna watu
wanajaribu kutumia kila fursa inayopatikana
kujinufaisha kwa kupata fedha hata ziwe
‘chafu’, kwao kitu cha maana ni kupata
utajiri kwanza.
Kundi la watu wanaofanya biashara ya
kusafirisha watu, wamekuwa wakitumia
fursa ya ukosefu wa ajira kama chambo cha
kuwanasa vijana na kuwaingiza kwenye
biashara haramu kama ukahaba.
Hivi karibu kundi hilo linalosafirisha watu
lilipita katika vyuo vikuu kadhaa nchini
Uganda na kuwaahidi wanafunzi kuwa
lingewatafutia kazi Ulaya na Marekani,
kwani lina uzoefu wa kutosha na kazi hiyo.
Mmoja wa vijana ‘waliobahatika’ kupata
nafasi ya kwenda Ulaya kufanya kazi ni
Sunday Bekunda (25), mwanafunzi wa
mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha
Makerere, Kampala.
Kwa bahati mbaya ‘neema’ ya kwenda
Ulaya iligeuka balaa baada ya kutekwa na
kulazimishwa kufanya ngono na wanawake
mbalimbali huku akirekodiwa kwenye
kamera za video.
“Ilikuwa ni Januari 2013, nilipokutana na
mwanaume mmoja anayeitwa Charles
kutoka katikati ya Jiji la Kampala, ambaye
aliniahidi kunipeleka Kenya kufanya kazi
katika kiwanda.
“Sikujua kuwa Charles alikuwa msafirisha
watu. Alikuwa anaonekana kama mzazi wa
makamo aliyefanya kazi kwa miaka mingi.
“Nilifungua moyo wangu na kumweleza
changamoto nyingi ninazopitia na namna
nilivyo hangaika kutafuta kazi ili nipate
fedha za kulipia masomo ya ziada. Kwa
kifupi ni kama nilikuwa namwambia Charles
kuwa sikuwa natafuta kazi bali nilikuwa
nataka kazi yoyote.”
Safari ya Kenya
“Siku iliyofuata nilikuwa tayari kwa safari na
nilimkuta Charles akiwa kwenye gari la
binafsi aina ya Toyota Noah. Alikuwa
pamoja na wasichana sita na wavulana
wawili. Alituambia kuwa tutaingia Kenya kwa
kupitia mpaka usio rasmi unaoitwa
Chepskunya.
“Tukiwa njiani, Charles alikuwa anaongea
sana na kutusisitizia kuwa ‘tusimwangushe’
tukifika huko. “Tulipofika Kenya
walituchukua na kutuingiza kwenye nyumba
moja nzuri ya makazi ya watu, hapo
tulikutana na wenzetu 15, wavulana wawili
kutoka Rwanda na Wakenya 13.”
Kutekwa
“Charles alituacha hapo tukiwa chini ya
mwanamke mmoja na wanaume wanne
wenye miili iliyojengeka vyema. Watu hao
walianza kutupiga makofi na kutulazimisha
tuvue nguo. Ndipo nilipobaini kuwa
kilichoonekana kama ni safari sasa imegeuka
utekaji.
“Baada ya kupigwa tuliambiwa tutoe
mifukoni kila kitu tulichokuwa nacho na
kuweka juu ya meza. Nilishtushwa nilipoona
vyeti vya wanafunzi wa Uganda kutoka Vyuo
Vikuu vya Kyambogo, KIU (Kampala
International University), Nkumba na UCU
(Uganda Christian University). Hata vyuo vya
Kenya vilikuwapo.
“Mwanamke alitutishia kutuua kama
tusingetii walichosema. Kudhihirisha
alichokuwa anamaanisha, alituonyesha
mkanda wa video wa mtu akiuawa na
kupasuliwa tumbo.
“Halafu wakaweka video vyingine
iliyotuonyesha biashara tutakayokuwa
tunaifanya, ambayo ni kuigiza picha za
ngono.”
Ratiba ya kufanya ngono
“Walituongoza hadi ghorofa ya juu na
kutuweka katika vyumba tofauti. Katika
chumba nilichokuwepo aliingia mtu na
kuniambia nitoe nguo kisha akanipa chupi
tatu zinazobana.
“Hicho chumba kilikuwa na mwanga mkali
na kamera za CCTV katika kila kona.
Baadaye wakamleta Bridget, mmoja wa
wasichana niliotoka nao Uganda, kisha
wakaniambia kuwa nipo huru kufanya naye
ngono. Walipoondoka na kufunga mlango,
Bridget alianza kulia na kupiga kelele.
“Matukio mabaya yalianza rasmi siku
iliyofuata wakati yule mwanamke alipoingia
kwenye chumba changu akiwa ameshika
mikanda mitatu ya ngono. Baadaye
waliletwa wanawake na wanaume niliokuja
nao nikaambiwa nifanye nao ngono wakati
watu wengine wakirekodi kwa kutumia
kamera kubwa.
“Nilipoishiwa nguvu, yule mwanamke alitoka
nje na kurudi halafu alinichoma sindano
yenye dawa ambayo ilinifanya nipate nguvu
tena na kuendelea. Nikapewa ratiba ya
kulala na wanawake asubuhi, wavulana jioni
(mashoga) na wanawake watu wenye umri
mkubwa usiku.
“Wanawake hao walikuwa wanawalipa wale
jamaa ili tufanye nao ngono. Kuna wakati
nilikuwa nalazimishwa kulala na wanawake
saba kwa siku huku nikipata maumivu
makali.”
Mauaji
“Baada ya wiki tatu wote tuliitwa sebuleni
na kupewa taarifa kuwa mmoja wetu,
aliyeitwa Sam Muteesi kutoka Uganda,
alikuwa amekataa kuwatii kwa hiyo alitakiwa
auawe mbele yetu. Walimfunga kwenye kiti,
japokuwa alikuwa akiomba sana msamaha
walimfunika usoni kwa kutumia begi hadi
alipokufa.
“Kwa kipindi chote cha Januari na Februari
2013, nilikuwa nikifanya ngono za kila aina
kila siku huku nikitumia dawa za kulevya na
pombe.
“Mwanzoni mwa Machi, Charles alikuja
kwenye chumba changu na kuniambia kuwa
ninatakiwa kwenda kuoa Uingereza. Halafu
akafungua kompyuta yake na kunionyesha
picha ya mwanaume mzee mzungu.
“Akaniambia nipite mbele ya kompyuta hiyo
nikiwa nimevaa chupi nilizopewa ili huyo
mzungu anione (kupitia Skype) kama nifaa.
“Huyo mzungu alinipenda, hivyo Charles
akawa amepata ‘dili’ ambayo ingenipeleka
Uingereza, lakini kwa kuwa sikuwa Mkenya
nilitakiwa nirudi Uganda kuchukua hati ya
kusafiria.
Atoroka
“Wakati tukivuka mpaka kuingia
Uganda, nilifanikiwa kukimbia pale Mbale
tulipokuwa tumesimama kunywa chai.
Nilitoa taarifa yangu na kufunguliwa faili
namba SD REF 65/19/03/2013. Kwa kuwa
Charles alikuwa mtu mwenye nguvu
(kifedha) hakufanywa chochote.
“Kutokana na mateso niliyopitia nilikuwa
kama kichaa, nililazwa katika Hospitali ya
Vichaa ya Butabika na nilipewa matibabu
kati ya Agosti na Desemba 2013.
“Pia nilipimwa vipimo vingine na
kugundulika kuwa nilikuwa na maambukizi
yote makubwa ya magonjwa ya
zinaa.“Nimeamua kusimulia habari yangu
kama sehemu ya kampeni ya kuwaonya
vijana wa vyuo vikuu kuwa makini na watu
wanaowaahidi kuwatafutia kazi nje ya nchi.”
Imeandaliwa na Goodluck Eliona kwa
Msaada wa Redio Netherlands Worldwide
(RNW)

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni