Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Saturday, August 9, 2014

Stori: Imelda Mtema
MAJANGA! Baada ya kuchomoka kwenye ule
msala wa awali wa madawa ya kulevya,
video queen matata Bongo, Agness Gerald
‘Masogange’ amejikuta akiteseka kwa ishu
hiyo kwa mara nyingine.
Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia Risasi
Jumamosi, Masogange alipatwa na msala
huo mara baada ya kutua katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar
hivi karibuni akitokea nchini Afrika Kusini
‘Sauz’ ambapo alidakwa na polisi wa kitengo
cha kudhibiti madawa ya kulevya nchini
kilicho chini ya Godfrey Nzowa.
Akisimulia ishu hiyo, Masogange ambaye
umaarufu wake mkubwa ulizaliwa katika
video ya Wimbo wa Masogange wa
Abednego Damian ‘Belle 9’, alisema
alikamatwa na watu wa uhamiaji nchini
baada ya kuhisiwa kuwa hati yake ya
kusafiria ina matatizo.
“Walinikamata baada ya kuiona hati ilikuwa
na ule msala wa awali lakini walinihoji na
nikawapa majibu ambayo yaliwaridhisha,
wakaniachia.
“Hii ishu inanitesa sana lakini nashukuru
Mungu kwa kuwa nakamilisha taratibu za
kuwa raia wa Afrika Kusini, nitaishi kule,”
alisema Masogange alipobanwa na Risasi
Jumamosi.
Juzi wakati gazeti hili likienda mitamboni,
Masogange alikuwa kwenye Ubalozi wa Sauz
nchini katika harakati za mwisho
kukamilisha taratibu za kuwa na uraia wa
Afrika Kusini ambako amesema ndiko
atakapokuwa akiishi.
Julai 9, mwaka jana, Masogange alikamatwa
na madawa ambayo yalihisiwa kuwa ni ya
kulevya nchini Afrika Kusini, akashikiliwa na
polisi kwa miezi kadhaa.
Septemba, mwaka jana Mahakama ya
Kempton ya jijini Johannesburg, baada
uchunguzi kukamilika na kubainika kuwa
hayakuwa madawa ya kulevya bali ni
kemikali zinazotengenezea madawa ya
kulevya, Masogange alitakiwa kulipa faini ya
R30,000 (Sh4.8 milioni), akawa huru.

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni