Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Friday, August 29, 2014


Kimenuka! Mama mmoja mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam,
aliyejitambulisha kwa jina la Mama Zahara, ameibuka na madai mazito
akimtuhumu msanii wa filamu ambaye pia ni mjasiriamali, Lulu Mathias
Semagongo ‘Anti Lulu’ kumtumia ‘SMS’ za usagaji mwanaye aitwaye Zahara,
Ijumaa lina kisa na mkasa.
Mama huyo, akiwa amefura, alitinga kwenye Ofisi za Magazeti Pendwa ya
Global Publishers zilizopo Bamaga-Mwenge jijini Dar, mapema wiki hii na
kueleza kuwa amebaini mchezo mchafu unaoendelea kati ya binti yake
ambaye ni denti wa kidato cha pili na Anti Lulu.
MSIKIE MAMA MWENYEWE
Akizungumza kwa hasira, Mama Zahara aliwaka: “Mimi nina mtoto huyu tu wa
kike, anasoma boarding huko Tanga lakini hivi karibuni alirejea akidaiwamepewa likizo ya wiki moja.
“Tangu huyu mtoto amekwenda boarding, nimebaini amebadilika sana,
amekuwa na vijitabia ambavyo sivielewi hivyo nikawa namchunguza sana.
“Leo (Jumanne wiki hii) wakati niko jikoni nikasikia anaongea na mtu akiwa
chumbani kwake, mazungumzo yale yalinitia shaka kwani kuna muda
nikamsikia ‘akimkisi’ aliyekuwa anazungumza naye.
“Nilihisi kitu f’lani lakini nikasema nitamvizia nichukue simu yake nikiamini
kama kuna kinachoendelea nitagundua, na kweli, alipotoka kwenda bafuni
nikaichukua simu yake na kukutana na mambo ya ajabu.
“Nilinasa hizi sms ambazo zilinionesha waziwazi kwamba mwanangu
anafanya vitendo vya kisagaji. Niliumia sana hasa ukichukulia kwamba nina
binti huyo tu.“Nilipoichukua ile namba, nikataka kujua kama kweli alikuwa
anachati na msichana mwenzake au mwanaume, ikabidi nifanye kama nataka
kumtumia pesa kwenye simu yake na hapo ndipo likaja jina la Lulu
Semagongo.
“Nilishtuka kwani namjua huyu msanii tangu alipokuwa mtangazaji.
Nilipompigia akanijibu kwa kifupi tu kwamba nimlee vizuri mwanangu na yeye
hawezi kumfanyia vitendo hivyo, nikaona bora nije kwenu mtanisaidia.”
MESEJI ZENYEWE ZIKOJE?
Zahara: Natamani kufanya kale kamchezo, unaweza kunisaidia?
Anti Lulu: Nitumie pesa!
Zahara: Kiasi gani cha pesa? Pesa siyo tatizo, umenielewa lakini? Nataka
tu…(kitendo kichafu).
Anti Lulu: Nitumie hiyohiyo, kwa muda huu nitumie 30,000.
Zahara: Sawa halafu tunaonana vipi?
Anti Lulu: Nitumie pesa muda huu, Jumamosi.
Zahara: Mbona mbali sana mpenzi, leo haiwezekani au hata kesho, pesa siyo
tatizo.
Anti Lulu: Nitumie pesa basi.
Zahara: Subiri kidogo baby, simu yenye pesa iko kwenye chaji, usijali,
nashukuru kwa kunionea huruma.
Anti Lulu: (kimya).
KESHO YAKE
Anti Lulu: Umeona ishu kunidanganya siyo?
Zahara: Siwezi kukudanganya mpenzi, ndiyo naamka nitakutumia ila usije
ukanidanganya maana nina..., hiyo Jumamosi tunaonana wapi?
Anti Lulu: Tuta-meet (kukutana) Bondeni Hotel (ipo Magomeni, Dar), basi
nitumie hiyo pesa.
Zahara: Nikutumie kwenye namba hii, vipi tutatumia vifaa?
Anti Lulu: Nitumie kwenye namba hii.
Zahara: Nijibu basi kama tutatumia vifaa au hivihivi…
Anti Lulu: Hakuna haja ya vifaa, mimi natosha…
Zahara: Haya natuma, nitafurahi sana.
Baada ya maelezo ya mama huyo kisha kuziona sms hizo, kweli zilionesha
Zahara ndiye aliyekuwa akimshawishi Anti Lulu amfanyie kamchezo hako
huku msanii huyo naye akionesha kuujua na kutaka apewe kwanza Sh.
30,000.
Kama ilivyo ada ya gazeti hili kutoa nafasi kwa mtuhumiwa kusikika, Ijumaa
lilimsaka Anti Lulu ili kupata maelezo yake ambapo alikuwa na haya ya
kusema:
HUYU HAPA ANTI LULU
“Kusema ukweli huyo binti ndiye aliyekuwa akinisumbua kwa kunitumia sms
za kunitaka.
“Alionekana kuuzoea na kuupenda sana sana huo mchezo, mimi sijawahi, ni
two different things (vitu viwili tofauti).
“Inavyoonekana alitaka kunichafua kwani alinilazimisha sana, sijawahi
kufanya huo mchezo na wala sifikirii hasa kwa binti kama mimi ambayenaamini wapo wanaume wanaonipenda, niingie kwenye usagaji natafuta nini?
“Huyo binti mwambieni anikome kabisa.”
KUTOKA MEZA YA IJUMAA:
Ni vyema wazazi wakawa na utaratibu wa kuwafundisha watoto wao juu ya
madhara ya kujihusisha na vitendo haramu kwenye jamii ili wawe na mwanga
wa maisha yao ya baadaye na hasa viongozi wa kesho wa taifa letu.
GPL

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni