Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Saturday, August 9, 2014

MAMBO WASIYOYAPENDA WANAUME WENGI..


1. Wanaume hawapendi kuambiwa cha kufanya na wenzi wao

Mwanamke unapotaka mwanaume afanye jambo usimwambie alifanye bali fanya kama una mpa ushauri. Kwamba John hivi kwa nini tusiweke balbu hapa kwenye korido maana kuna giza kweli. Badala ya hivi wewe John huoni hapa kwenye korido kuna giza balbu imeungua mwezi sasa hujabadilisha kwa nini? Weka balbu bwana. Atafanya au asifanye kabisa kwa sababu umemwambia cha kufanya.

2. Wanaume hawapendi mwenzi mwenye makelele, mlalamishi

Yeye ni kulalamika kuanzia Jumatatu hadi Jumapili. Japo wanawake nao wanasema kuna wanaume walalamishii balaaa. Na wenye gubu wanasusa kula mpaka kuongea wanawanunia wake zao mmmmh!

3. Wanaume hawapendi mwenzi mchafu

Mchafu wa mwili wake na hata nyumbani kwenye suala la kutunza nyumba wanayoishi. Uchafu hufanya mwanamke apoteze mvuto.

4. Wanaume hawapendi mwenzi mbishi

Japo na wanawake wanasema wanaume ndio wabishi zaidi. Utampa mwanaume ushauri lakini haufanyii kazi ubishi mwingi.

5. Wanaume hawapendi kuamrishwa na mwenzi wao

Mwenzi mbabe anaetoa amri na kumtawala hawataki.

6. Wanaume hawapendi kuhisiwa hisiwa na kusachiwa sachiwa
Kumpekua kwenye simu, mifuko ya suruali kwamba unamulika mwizi. Hawapendi, tena pengine hawajafanya jambo la kuwafanya wahisiwe vibaya.

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni