Kundi la la wapiganaji wa Kiislamu la Iraq na Syria (ISIS) limetekeleza mauji ya kutisha kwa kumkata kichwa mwandishi wa habari wa Marekani.
Mwandishi huyo ambaye pia ni mpiga picha mashuhuri aliyetajwa kwa jina la James Wright Foley alikamatwa na wanajeshi wa kundi hilo mwaka 2012 nchini Syria alikokuwa akiripoti habari za kuondolewa madarakani Bashir Al-Assad.
Katika video inayoonesha mauaji hayo iliyowekwa YouTube inamuonesha mtu aliyemkata kichwa mwandishi huyo akiwa amejifunika uso kwa mask akiongea kiingereza kwa lafudhi ya Uingereza, akidai kuwa wanafanya hivyo kama sehemu ya kulipiza kisasi kwa rais Obama aliyetoa amri ya mashambulizi ya anga dhidi ya kundi hilo nchini Iraq.
Msemaji wa ISIS, ameonya kuwa kutakuwa na tukio lingine la kulipiza kisasi kwa kumkata kichwa mwandishi wa Marekani Steven Sotloff wanaemshikilia
0 comments:
Post a Comment