
Juzi wakati msanii Fareed Kubanda - Fid Q yuko ndani ya XXL ya Clouds fm
anatambulisha ngoma yake mpya inaitwa Bongo Hip Hop, mtangazaji Adam
Mchomvu amekuwa anambana na maswali sana kiasi cha Fid kumtolea uvivu
kuwa "najua umeagizwa kuja kuni-harass kwenye interview yangu".
Adam alikuwa anambana sana na maswali ya kwa nini amerudia ngoma hii
kutoka Tongwe Records aliyomshirikisha Juma Mohamed Mchopanga (Jay
Moe) na kuirudia Bongo Records akimshirikisha P.Funk Majani?
Adam anaonekana kumind hii kitu kiasi cha kulazimisha kuipiga ngoma ile
version ya mwanzo ya Tongwe baada ya hii version ya Bongo Recz
kumalizika (ingawa kibishi sana maana B12 alikuwa anataka kubana. Ila kabla
ya ngoma kuisha B12 akaikata na Adam anasikika akimind na kusema kesho
atashusha mzigo mwingine.
Kilichonipa maswali hapa ni Je Adam ni ile loyalty yake ya kuwa Record Label
kule Tongwe Records ama ana ubia kule Tongwe ndiyo sababu ya
kuishupalia hii kitu namna hii? Hebu mwenye idea na hii kitu atujuze wadau.
0 comments:
Post a Comment